Serikali yakusanya Tsh. Trilioni 13.6 Julai hadi Januari 2023

Serikali yakusanya Tsh. Trilioni 13.6 Julai hadi Januari 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya Sh13.601 trilioni ya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi katika kipindi cha Julai 2022 hadi Januari 2023, sawa na asilimia 98.8 ya lengo la kukusanya Sh13.763 trilioni.

Hayo yamebainishwa kwenye taarifa ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya mwaka 2023/24 iliyotolewa leo Machi 13, 2023 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba aliyeuwasilisha kwa wabunge jijini Dodoma.

Taarifa hiyo inaonyesha kwamba kati ya mapato hayo, mapato ya kodi yalikuwa Sh12.809 trilioni na mapato yasiyo ya kodi ni Sh791.4 bilioni. Vilevile, katika kipindi hicho, jumla ya Sh642.2 bilioni zilitumika kulipa marejesho mbalimbali ya kodi.

“Kati ya marejesho hayo, Sh524.9 bilioni ni marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Kutofikiwa kwa lengo kulitokana na baadhi ya wafanyabiashara wasiokua waaminifu kuendelea kutumia mbinu mbalimbali kukwepa kodi,” inaeleza taarifa hiyo.

Katika kipindi kilichobaki hadi Juni 2023, Serikali imeahidi kuendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha ukusanyaji wa kodi ili kufikia malengo, zikiwemo kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mipaka yote nchini kwa kufanya doria za mara kwa mara ili kudhibiti ukwepaji kodi na biashara za magendo.

Pia, inakusudia kushirikisha Taasisi za Serikali katika kusaidia urejeghaji wa madeni ya kodi kutoka kwa wauzaji wa bidhaa na huduma kwa taasisi za umma.

“Serikali itaendelea na kampeni mbalimbali nchini za kutoa elimu kwa mlipakodi kupitia semina, makongamano na vyombo vya habari kwa lengo la kupata maoni juu ya njia bora ya kuwahudumia ili kuongeza uhiari wa kulipa kodi,” inaeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inabainishaa kwamba mapato yasiyo ya kodi kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Januari 2023, yalifikia Sh1.461 trilioni ikiwa ni asilimia 84.6 ya lengo la kukusanya Sh1.728 trilioni.

“Kati ya makusanyo hayo, Sh975.7 bilioni zilitoka kwa Wizara na Idara zinazojitegemea na Sh485.7 bilioni ni mapato yatokanayo na michango na gawio kutoka kwenye Taasisi na Mashirika ya Umma.

“Kutokufikiwa kwa malengo ya ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kulitokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mwitikio mdogo wa wamiliki wa ardhi kulipa ada na tozo za ardhi kwa wakati,” inabainisha taarifa hiyo.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom