Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Kauli hii imetolewa bungeni na naibu waziri wa afya Bwana Moleli. Amesema serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa Cha pesa kugharamia wajawazito. Hii imekuja wakati baadhi ya wabunge walipotaka kujua ni upo msimamo wa serikali dhidi ya kauli za baadhi ya viongozi kwa wananchi hasa wajawazito.
My take: Rasimi serikali imeamua kujitoa ufahamu na kukaa upande wa watesi wetu. Hivi billion 227 serikali inaona ni pesa nyingi za kushindwa kuhudumia wizara ya afya? Yale mabilioni ya kuwalipa wasanii waliokwenda Korea kujifunza filamu nani aliyaidhinisha?
Zile pesa za kugharamia safari za wasanii kwenye Kila kikao Cha chama nani ameidhinisha? Yale mabilioni ya pesa aliyochukua Bashe kwa kisingizio Cha BBT nani ameyakagua na kuifhinisha? Zile pesa za bakishishi kwa timu za simba na yanga maarufu kama goli la mama nani ameidhinisha? Ile milioni 700 walizopewa wachezaji wa timu ya taifa nani aliidhinisha?
Kwanini tunakuwa kama tumechanganyikiwa ?
Soma: Mbunge ahoji kauli ya serikali kuhusu wanawake wanaokosa vifaa vya kujifungulia, Naibu waziri asema huduma kwanza na si kuulizwa pesa