Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mitaa ina furaha, Raha, Amani, Tabasamu na matumaini makubwa sana. Hii ni Baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya kilimo ya Takribani billioni Mia Tisa na sabini iliyoleta Nuru na Mwanga kwa wakulima,Sasa Taifa ni Nuru tupu na mwanga kila eneo.
Ikumbukwe ya kuwa kilimo Ni secta iliyo ajiri na kutoa ajira kwa mamilioni ya watanzania,Hivyo ukiinua,kukiwezesha na kukipa kipaombele kilimo unakuwa umeinua ,kuwezesha na kuyapa kipaombele maisha ya mamillioni ya watanzania,unakuwa umewapa pumzi Safi,unakuwa umeleta nuru na Tabasamu Katika Mioyo ya watanzania.
Unakuwa umeinua maisha na kipato Cha mtanzania,unakuwa umeliinua Taifa ,unakuwa umechochea biashara mitaani na kuupa Afya mzunguko wa fedha.kwa kukiinua kilimo unakuwa umekuza secta ya viwanda,unakuwa umepunguza umaskini kwa Kaya nyingi,unakuwa umeboresha maisha ya watanzania,unakuwa umepunguza utegemezi,unakuwa umetoa ajira kwa vijana, kuleta Furaha kwa vijana na unakuwa umeongeza mapato ya ndani pamoja na fedha za kigeni.
Mikakati na mipango ya serikali katika kilimo imewakosha wakulima na watanzania kwa ujumla wao.Sasa Tanzania inakwenda kusambaza na kulilisha Bara Zima la Afrika,Sasa Tanzania inakwenda kuwa kimbilio la wote wenye njaa kutoka kila pembe ya Afrika. Njaa imeagwa rasmi katika uongozi huu wa Rais Samia,mfumuko wa Bei ya vyakula unakwenda kubakia historia katika makaratasi.
Watanzania tunakwenda kushuhudia ukuaji na uanzishaji wa viwanda kutokana na kuwepo kwa malighafi ya kutosha,tunakwenda kushuhudia ongezeko la ajira kwa vijana, Tunakwenda kuona mzunguko wa fedha wenye Afya imara, tunakwenda kushuhudia umaskini wa kipato ukipungua kwa watanzania kwa kuwa secta inayogusa maisha ya watanzania wengi imeguswa na kupewa kipaombele,tunakwenda kuona mapato ya mwezi yakiongezeka pamoja na kuona maisha Bora kwa kila mtanzania yakitimia na kila mmoja akitimiza Ndoto zake za kiuchumi.
Kwa hakika Rais Samia Mama yetu na serikali yake wametambua Ni wapi pakukamatwa ili kuutokomeza na kuukausha mzizi wa umaskini. Haya yanayofanywa na Rais Samia Ndio hushauriwa na wanauchumi nguli juu ya kuwekeza katika secta yenye kuleta tija kwenye maisha ya wengi.Rais Samia anatimiza Ndoto za Baba wa Taifa na kwa hakika Ni Kama Hayati mwalimu Nyerere Amezaliwa ndani ya Rais Samia.
Rai yangu ni kuiomba Tu serikali yetu ihakikishe inatoa fedha zote Kama zilivyopitishwa na Bunge letu katika Wizara hii ya kilimo ili kufanikisha mipango Yake mizuri inayokwenda kuleta Tabasamu , matumaini na furaha katika maisha ya watanzania pamoja na kuchochea mapinduzi ya kilimo na viwanda hapa nchini.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.