Serikali yalifunga kanisa la EAGT Moshi kutokana na mgogoro wa Viongozi na Waumini

Serikali yalifunga kanisa la EAGT Moshi kutokana na mgogoro wa Viongozi na Waumini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
0c05c38706c8933a223827ac0c0e577d

Serikali ya Wilaya ya Moshi imelifunga kwa muda kanisa la Evangelist Assembles of God (E.A.G.T) Mawenzi lililopo Mtaa wa Vigae kutokana na mgogoro kati ya waumini na uongozi wa juu wa kanisa.

Chanzo cha mgogoro kinadaiwa kuwa ni uongozi wa juu wa kanisa hilo kumuondoa mchungaji mwanzilishi wa kanisa hilo katika mtaa huo, Frank Mushi na kumleta mchungaji mwingine pasi na ridhaa ya waumini.


0c05c38706c8933a223827ac0c0e577d-1


Uongozi wa kanisa umesema sababu ya kumuondoa mchungaji huyo ni kutokuwa na elimu ya dini (theology), hivyo hajakidhi vigezo vya kutoa huduma kwa waumini.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo amesema kuwa uongozi wa kanisa ulikimbilia polisi, badala ya kumaliza mgogoro huo ndani ya kanisa kwa sababu wanataka kutumia nguvu kuleta mchungaji mpya na kumuondoa yule aliyekuwepo.

“Walikuja kutupa nje vyombo vya mchungaji na mchungaji akaondoka. Sisi tukabaki hapa kanisani tukiomba Mungu atausaidie, sasa sijui imefikaje huko kwa mkuu wa wilaya, na wakamshtaki mchungaji na makosa ya uongo. Sasa leo tukiwa tunasali, magari ya polisi yakaja, yakafunga,” amesema muumini huyo.

Amesema si kweli kwamba mchungaji huyo amekataa kwenda shule kusoma elimu ya dini kama ambavyo uongozi wa kanisa umedai, lakini alishindwa kwenda kwa sababu wakati wanamtaka aende alikuwa amevunjika mkono.

“Wanasema wamemfukuza kwa sababu amekataa kwenda kusoma Bible School (Shule ya Biblia), halafu na kipindi hicho alikuwa amevunjika mkono, na hadi sasa ni miaka 16 mkono haujaunga. angeenda vipi,” amehoji mmoja wa waumini.

Mbali na hilo, baadhi ya waumini wamedai kuwa sababu nyingine ya mchungaji wao kuondolewa ni nia ovu ya uongozi kutaka kuwageuza wao kama sehemu ya biashara kwani mchungaji aliyekuwepo alikuwa akitumia sadaka kujenga makanisa maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro.

Wakati Frank Mushi anafukuzwa alikuwa tayari amepanda ngazi ya uongozi na kufikia kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Kilimanjaro.
 
Chuki huzaa chuki, na mwishowe kukumaliza wewe mwenyewe, kila siku shida tu pande hizo, hakuna good news!
 
Tatizo hapo ni sadaka, chanzo ni maslahi.
Hapo dawa ni moja tu, waumini wasepe zao kwenda kufanya mambo mengine ya kimaendeleo binafsi. Waumini wasikubali kuwa watumwa wa makanisa, wakati makanisa mengi ni miradi ya watu binafsi au vikundi fulani.

Mungu yupo popote pale ukimwamini.
 
Kanisa la EAGT lilianzishwa katikati ya mazingira ya migogoro, ni zao la migogoro. Hivyo matunda makuu ya uwepo wa hilo kanisa yatakuwa ni migogoro, migogoro. Historia wa kipentekoste hapa Tanzania inalitaja hivyo kanisa la EAGT.
 
Anapo hamishwa ni kuimalisha utendaji kazi wake. Yeye akubali kwenda masomoni ili kuepusha mengi, ikishindikana waumini waende katika Imani zingine.
 
watu wa mungu hutatua mambo kwa misingi ya upendo na aman,kufikia stage hiyo ujue kuna tatizo kubwa ndani ya hilo kanisa...haya matatizo ya kikanisa yapo tu,kila kanisa huwa lina migogoro yake,ya chinichini ila inategemea na namna ya njia inayotumika katika utatuzi wa migogoro yao....
 
By: SEREKALI ya wilaya- Moshi kama ktk tangazo bila nukuu ya rejea / reference ya barua yenye amri /katazo ?!

0c05c38706c8933a223827ac0c0e577d


Serikali ya Wilaya ya Moshi imelifunga kwa muda kanisa la Evangelist Assembles of God (E.A.G.T) Mawenzi lililopo Mtaa wa Vigae kutokana na mgogoro kati ya waumini na uongozi wa juu wa kanisa
 
Mchungaji miaka 16 kavunjika mkono, wakati kila siku nyie wakristo mnatamba kuponya, imekuaje kwa mchugaji? Au mganga hajigangi?
 
MCHUNGAJ ALIETOLEWA NI MANGI. SASA JE, ALIELETWA NI KABILA GANI? HEBU KWANZA WEKENI WAZI MAANA KUNA JAMBO LA KUJADILI HAPO.
 
Hivi na Daimond naya bado hajatimuliwa kwenye msikiti aliojenga?
 
Unaweza kujiuliza mchungaji katumwa anzishe Huduma sehemu sasa huyu mtu kapigana mungu kamsaidia kakusanya waumini wengi kajenga Kanisa zuri waumini wakamnunulia na gari mchungaji zuri mchungaji wao Huduma ikakua.sasa utashangaa uongozi Wa Kanisa toka jimboni wanamuondoa wanampeleka kwingine bila ridhaa ya mhusika hili sio zuri
 
Back
Top Bottom