Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hoja la malalamiko ya awali ilitolewa Mei 25, 2024, kuisoma bofya hapa ~ Tabora – Uyui: Wananchi waliotakiwa kupisha Mradi wa SGR waomba Serikali isaidie walipwe fidia zao
Imeelezwa kuwa Wananchi hao wamelipwa stahiki zao mapema mwezi huu na tayari wameanza mchakato wa kuvunja makazi yao ili kuhama na wengine tayari wamehama.
Awali, Wananchi hao walidai licha ya kufanyiwa tathimini tangu Machi 2023, hawakupokea malipo hadi Mei 2024 na hawajui hatima ya malipo yao.
Mei 30, 2024, Siku chache baada ya JamiiForums.com kuripoti suala hilo, Mbunge wa Igagula, Venant Daud Protas alihoji juu ya hatma ya malipo ya Wananchi hao Bungeni, alielekeza swali hilo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lakini Spika Tulia Ackson akasema hilo swali linapaswa kuelekezwa kwa Wizara husika.
Kusoma na kuangalia hoja ikiulizwa Bungeni, soma - Mbunge ahoji ukimya wa Serikali kuhusu fidia ya waliopisha Reli ya SGR Tabora
Akizungumzia taarifa hiyo, Diwani wa Kata ya Nsololo, Habibu sungwa alisema “Ni kweli wameshalipwa na tayari wameanza kuondoa vitu vyao, wamepewa wiki mbili za kukamilisha mchakato wao kwa hiyari.”
Pia soma ~ Mkuu wa Wilaya: Wananchi wa Uyui wanaodai malipo ya kupisha Mradi wa SGR wafike ofisini