Serikali yamfungia masanii Roma Mkatoliki Kujihusisha na Muziki kwa miezi 6

GfreyNang

Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
16
Reaction score
23
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza leo Machi 1, 2018 na baadhi ya wasanii aliowaita na kuwaeleza dosari zilizopo katika nyimbo zao, Shonza amesema baada ya Roma kupewa muda wa kufanya marekebisho wimbo wake wa Kibamia ameshindwa kutekeleza agizo hilo.

“Mpaka sasa hajaufanyia marekebisho na wimbo huo unaendelea kurushwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Tulitoa muda kwa Roma kufanyia marekebisho wimbo wake tangu mwaka jana mwishoni lakini mpaka leo ni miezi mitatu ameshindwa kutekeleza hilo,” amesema Shonza.

Amesema jana msanii huyo alipigiwa simu ili leo afike katika kikao hicho kwa ajili ya kujitetea, pia hakutokea.
 

Attachments

  • vlcsnap-8293-11-21-22h05m19s528.jpg
    48 KB · Views: 92
Sasa hivi kila msanii aanze kuimba nyimbo za kuisifia serekali na viongozi wake
 
Kwani inafungiwa nyimbo au yeye, kama sijakosea wahusika wa hiyo nyimbo ni wawili.Why Roma?
Wanamuziki wengi nyimbo zao zilifungiwa pasipo wao kufungiwa kufanya kazi za muzic kwanini huyu!

Mungu ibariki nchi yangu.
 
Na kwa nn isiwe Rostam akawe Roma huo wimbo ni wa kundi ilipaswa liadhibiwe kundi na sio member mmoja lbda kama ana makosa mengine binafsi nje ya kundi.
 
Mambo ya kijinga,mbona wimbo ni wa siku nyingi?kama kusikika umesikika vya kutosha kwa ujumla nyimbo zilizofungiwa nyingi zimedumu zaidi ya mwaka sasa hata aielewi lengo lao nini hasa!!
 
Hivi mbali ya kufungia nyimbo na wasanii huyo shonza kazi yake nyingine ni ipi?
 
HIVI WAMEWAFUNGIA ROMAN CATHOLIC KUIMBA KWAYA?INA MAANA KWAYA ZA ROMA ZINAKASHIFU NINI???
Afu hii bangi sio nzuri asee
 
Hivi mbali ya kufungia nyimbo na wasanii huyo shonza kazi yake nyingine ni ipi?
kazi yake nyingine nadhani ni kufuatilia udaku tuu,leo CHADEMA wamesema nini ajibizane nao esp humu JF mimi nilishasema huyu mdada hakubaliki sio tu na hao wasanii na wanamichezo lakini hata vijana kiujumla hatumtaki,hana jipya sio creative katika hii wizara ni mzigo... Juliana Shonza, bora Mhe. Rais angemshusha Nape ndo awe naibu waziri afadhali kuliko huyu mdada Juliana Shonza, mzigo wote tunaona anaubeba mhe.mwakyembe huyu mdada abaki tuu huku nje ajibizane na vijana wenzie mitandaoni tena nadhani angepewa kitengo cha kujibizana na mange kimambi huko insta
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Waache upuuzi, kama watu wanaimba kwa mafumbo waachwe waimba, hawajataja neno mbo** au ku** kwenye nyimbo.
 
Arudi kwenye harakati tu twende sawa. R.O.M.A na kibamia wapi na wapi? Nilimshangaa sana aisee. Kutoka kwenye uanaharakati hadi kuimba vibamia! Fungieni tu ili akili yake imrudi aanze kukushughulikieni
 
Reactions: UCD
Inamaana huo wimbo walishindwa kuuzuia tu ulipotoka?

The damage has been done, kwanza hata ukifungia utapita mtaani bodaboda anaupiga watu wanao kwenye simu zao.

Hebu nyie mliopewa dhamana ya kusimamia hiyo wizara acheni upuuzi na jikiteni zaidi kwenye kufanya mambo ya maana ya kimaendeleo. Sio kutafuta kiki kwenye mambo yakipumbavu
 
Jamaa kapewa haki yake hii nyimbo inaharibu jamii kabisa ukija mtaani utashangaa watoto wadogo wanavyomalizia tusi lake
 
Kuna mstari mmoja chokozi sana pale

nionyeshe utundu,..

nikulambe mpaka .......
 
BASATA pia wahakikishe Wasanii wanapata kinachowastahili kwa kufuatilia vitu kama hakimiliki sio tu kufuatilia wanakosea wapi kila siku
 
Na kwa nn isiwe Rostam akawe Roma huo wimbo ni wa kundi ilipaswa liadhibiwe kundi na sio member mmoja lbda kama ana makosa mengine binafsi nje ya kundi.
May be mistari aliyoimba roma ndo ilikiuka maadiri
 
Kwann basata wasiunde kitengo ambacho jukumu lake litakuwa kuzisikiliza/ kuangalia video za nyimbo fulan kabla ya kuwa released kwny media.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…