Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP

Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Dar es Salaam.

Serikali imemwekea pingamizi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika kesi yake kikatiba, ikitaja sababu nne na kudai kuwa kesi hiyo ni batili kwa kuwa ina upungufu wa kisheria.

Hivyo Serikali inaiomba mahakama hiyo iifute kesi hiyo bila kuisikiliza hoja za msingi.

Mbowe alifungua kesi hiyo ya kikatiba Julai 30 mwaka huu, Mahakama Kuu dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo namba 21 ya mwaka 2021, Mbowe anapinga utaratubu uliotumika kumkamata, kumweka kizuizini na hatimaye kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji John Mgetta, akishirikiana na Jaji Leila Mgonya na Jaji Stephen Magoiga, ilitajwa kwa mara ya kwanza Agosti 9, mwaka huu ambapo waidai waliomba siku 14 kuwasilisha majibu yao dhidi ya madai ya Mbowe.

Leo Agosti 30, kiongozi wa jopo la wadaiwa, wakili wa Serikali Mkuu Hangi Chang’a amekanusha madai ya Mbowe.
Wakili Kibatala kwa upande wake aliieleza mahakama kuwa baada ya kurejea mambo mbalimbali kuhusiana na kesi hiyo wameona kwamba hakuna haja ya kuwasilisha kiapo cha ziada.

Kutokana na pingamizi hilo la awali, kama ilivyo kawaida, mahakama imelazimika kusimamisha kwanza mwenendo wa kesi ya msingi na badala yake itasikiliza na kuamua kwanza pingamizi la Serikali.

Ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za pingamizi la Serikali, basi itaitupilia mbali kesi hiyo na hicho ndicho kitakuwa kifo chake.

Lakini kama mahakama itupilia mbali hoja za pingamizi la Serikali basi kesi hiyo itakwenda katika hatua ya pili ambayo ni usikilizwaji wa hoja za Mbowe katika kesi ya msingi pamoja na hoja za Serikali kuhusiana na madaia ya Mbowe na kisha itatoa uamuzi.

Katika usikilizwaji wa pingamizi hilo la awali, Wakili Chang’a aliomba ufanyike kwa njia ya maandishi maombi ambayo mahakama imekubaliana nayo baada ya mawakili wa Mbowe kueleza kuwa hawana pingamizi dhidi ya maombi ya Serikali ya kusikiliza pingamizi hilo kwa njia ya maandishi.

Jaji Mgetta ambaye atasikiliza na kuama pingamizi hilo aliwataka Serikali kuwasilisha hoja zake za maandishi Septemba 6 na Mbowe kuwasilisha majibu yake ya hoja za pingamizi la Serikali Septemba 9 mwaka huu.

Pia Jaji Mgetta aliiamuru Serikali kama itakuwa na hoja za nyongeza kuhusu majibu ya Mbowe, kuziwasilisha mahakamani Septemba 13 na akapanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Septemba 23, mwaka huu, saa Nane Mchana.

mbowe-pc-data.jpg


Chanzo: Mwananchi

Pia, soma;

 
Pia Jaji Mgetta aliiamuru Serikali kama itakuwa na hoja za nyongeza kuhusu majibu ya Mbowe, kuziwasilisha mahakamani Septemba 13 na akapanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Septemba 23, mwaka huu, saa Nane Mchana.
Hongera sana kwa uandishi huu.

Habari inaeleweka vizuri na lugha imenyooka vizuri kabisa.

'Mwananchi' waandishi wa maana namna hii ni hazina nzuri. Watuzeni.
 
Mfa maji haishi kutapatapa.
aache kesi ya msingi ingurume kama kweli yeye sio Gaidi, kwa nn anataka kesi ifutwe hata kabla ngoma haijachezwa?! anafahamu uovu wake wote utawekwa hadharani ni wananchi wataijua tabia yake ovu dhidi ya nchi hii.
 
P.O NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA MASHAURI KAMA HAYO, THE EXPECTED!
 
Mfa maji haishi kutapatapa.
aache kesi ya msingi ingurume kama kweli yeye sio Gaidi, kwa nn anataka kesi ifutwe hata kabla ngoma haijachezwa?! anafahamu uovu wake wote utawekwa hadharani ni wananchi wataijua tabia yake ovu dhidi ya nchi hii.
Wewe mwenye nia njema umeifanyia nini nchi hii?!!....watu walitumia damu na fedha kutafuta Uhuru wako Leo unaona wana tabia ovu?!!..uliwahi kusoma hata history kidogo?!!..
 
Wewe mwenye nia njema umeifanyia nini nchi hii?!!....watu walitumia damu na fedha kutafuta Uhuru wako Leo unaona wana tabia ovu?!!..uliwahi kusoma hata history kidogo?!!..
naipenda nchi yangu Tanzania, kamwe siwezi kufanya vitendo vyenye madhara au kuvunja AMANI ya nchi yangu ninayo ipenda.
ndio maana siku zote natetea Amani ya nchi yangu.
nawachukia sana wale wenye nia ya kuvuruga amani na utulivu wa nchi kama inavyo daiwa Mbowe na genge lake walivyo dhamiria.
 
Mbowe anafahamu uovu wake alio kuwa anutenda kwa kificho sasa anataka ajinasue kwa njia ya mkato ili uovu wake usitambuliwe na watu wengine. anaona aibu na fedha kwa kiongozi kama yu kufanya hayo aliyo kuwa akiyafanya dhidi ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom