Serikali yanunua Madume ya Ng’ombe 366 kwa Tsh. Milioni 878.4

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde amesema katika kipindi cha miaka miwili tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, serikali imenunua madume ya ng’ombe ya kisasa 366 yenye thamani ya Silingi Milioni 878.4 ili kuboresha mifugo nchini.

Silinde ameyasema leo katika Kata ya Dakawa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa hafla fupi ya kugawa madume 40 kwa vikundi vya wafugaji 20 ili kuboresha mifugo yao ya asili katika wilaya hiyo.

Amesema Rais Samia amekuwa akifanya kazi nzuri katika kipindi kifupi kwenye Sekta ya Mifugo akiwa na lengo la kuinua wafugaji nchini kwa kuwa na mifugo bora na kisasa.

Picha-na.-1-scaled.jpg

Mhe. Rais anapowanyanyua wafugaji anataka wananchi kuwa na maisha bora na amekuwa akihangaika katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.” Amesema Silinde
Amesema uwepo wa madume bora ya kisasa ya ng’ombe ambao wamesambazwa maeneo mbalimbali nchini, ng’ombe watakaotokana na madume hao watakuwa na nyama nyingi na kufungua fursa zaidi za upatikanaji wa nyama kwa wingi kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Afisa Mifugo Mkuu Basil Mataba amesema ng’ombe hao 366 wamegaiwa kwenye halmashauri nane katika mikoa minane ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambayo ina wafugaji wengi.

Mataba amebainisha kuwa licha ya ugawaji wa madume hayo kwa vikundi vya wafugaji lakini mafunzo yamekuwa yakitolewa namna ya kuwatunza na kufuatilia matumizi yake pamoja na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.

Picha-na.-1-1-scaled.jpg

Aidha, ametoa maelekezo ya namna vikundi vinapaswa kutunza madume hayo kwa kutotumiwa katika shughuli nyingine ikiwemo ya kilimo kwa kuwa serikali imenunua na kusambaza madume kwa vikundi vya wafugaji kwa ajili ya kupandishia ng’ombe jike pekee na vikundi haviruhusiwi kuuza madume hayo.

HABARI LEO
 
Nahisi issue ya katiba lazima itakuwa na kipengere cha utendaji plus uwajibikaji.

Hii ya serikali kununua assets na kuwakopesha wananchi wake alafu unarudi kusema "Mh. Rais amefanya hivi..., ili muwe na maisha bora..." Siyo sahihi.

Rais ni mtendaji wangu anayepaswa kutekeleza majukumu yake kwa lengo la kumfanya kila raia kupata mafanikio kupitia utendaji uliorahisishwa na aliowakasimisha uongozi.
 
Safi sana mama piga kazi kanyaga twende
 
Huku mjini dume linaweza lala 3.6m.
Kufuga ng'ombe sio mchezo😀 unatakiw ujipange kisawa sawa tena ufugaji huu wa kukatia majini...
NA kulisha pumba na mashudu sio?
 
Huu Wizi yani Ng'ombe moja 2.4 M
Khaa emb search ranch zenye madume ya Boran uone Bei zake Kama huja jikojolea hapo.

Ingia insta acc mbogo ranches uangalie Bei za madume ya Boran Kisha urudi tena hapa
 
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde amesema katika kipindi cha miaka miwili tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, serikali imenunua madume ya ng’ombe ya kisasa 366 yenye thamani ya Silingi Milioni 878.4 ili kuboresha mifugo nchini.

Silinde ameyasema leo katika Kata ya Dakawa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa hafla fupi ya kugawa madume 40 kwa vikundi vya wafugaji 20 ili kuboresha mifugo yao ya asili katika wilaya hiyo.

Amesema Rais Samia amekuwa akifanya kazi nzuri katika kipindi kifupi kwenye Sekta ya Mifugo akiwa na lengo la kuinua wafugaji nchini kwa kuwa na mifugo bora na kisasa.

Picha-na.-1-scaled.jpg

Amesema uwepo wa madume bora ya kisasa ya ng’ombe ambao wamesambazwa maeneo mbalimbali nchini, ng’ombe watakaotokana na madume hao watakuwa na nyama nyingi na kufungua fursa zaidi za upatikanaji wa nyama kwa wingi kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Afisa Mifugo Mkuu Basil Mataba amesema ng’ombe hao 366 wamegaiwa kwenye halmashauri nane katika mikoa minane ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambayo ina wafugaji wengi.

Mataba amebainisha kuwa licha ya ugawaji wa madume hayo kwa vikundi vya wafugaji lakini mafunzo yamekuwa yakitolewa namna ya kuwatunza na kufuatilia matumizi yake pamoja na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.

Picha-na.-1-1-scaled.jpg

Aidha, ametoa maelekezo ya namna vikundi vinapaswa kutunza madume hayo kwa kutotumiwa katika shughuli nyingine ikiwemo ya kilimo kwa kuwa serikali imenunua na kusambaza madume kwa vikundi vya wafugaji kwa ajili ya kupandishia ng’ombe jike pekee na vikundi haviruhusiwi kuuza madume hayo.

HABARI LEO
Hapa ninachoona mimi shida sio bei

Ila je hao madume wanaendana na hiyo bei maana picha za hao madume sijaziona

Unaweza kukutani wale waliokondeana ila title inaandikwa madume ili kuleta uzito ionekane ni yale mashababi.
 
Back
Top Bottom