Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeondoa ulazima wa kuvaa barakoa isipokuwa pale inapobidi, mfano kwa wale wenye magojwa ya mfumo wa hewa na kwenye mikusanyiko ya ndani.
Hii inatokana na kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19 nchini na Duniani kote.
Kulingana na mwenendo huu, Serikali imeamua kufanya yafuatayo;
Jumla ya visa 35,747 na vifo 808 vimethibika kuwepo nchini tangu kuripotiwa kwa mgonjwa wa kwanza mnamo Machi 2020
Hii inatokana na kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19 nchini na Duniani kote.
Kulingana na mwenendo huu, Serikali imeamua kufanya yafuatayo;
- Kuendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19
- Kuendelea kufanya uchunguzi wa afya dhidi ya magonjwa ya milipuko kwa wasafiri wa kimataifa katika viwanja ya ndege vya kimataifa, bandari na mipaka ya chi kavu. Aidha, matumizi ya vipimajoto (thermoscans) kuchunguza COVID-19 kwa wasafiri hao yamesitishwa.
- Kusitisha kufanya kipimo cha haraka (Rapid Test) kwa wasafiri wanaoingia nchini kutoka nchi zote wenye yeti ya chanjo ya UVIKO-19 au cheti cha RT - PCR.
- Kuongeza umri wa watoto kutoka nje ya nchi wanaotakiwa kusamehewa kupima UVIKO-19 kabla hawajaingia nchini kutoka umri wa miaka 5 (iliyokuwa awali) hadi miaka 12.
- Kuondoa sharti la kipimo cha RT-PCR kwa madereva wa malori na magari ya abiria yanayoingia nchini kwa waliopata chanjo ya UVIKO-19.
Jumla ya visa 35,747 na vifo 808 vimethibika kuwepo nchini tangu kuripotiwa kwa mgonjwa wa kwanza mnamo Machi 2020