Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza amesema Serikali imekubali mapendekezo ya wabunge ya kuondoa ushuru ya Sh382 kwenye gesi inayotumika katika magari.
Amesema hayo leo Juni 27,2024 wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2024.
Amesema kamati imefikia uamuzi huo kwa kuzingatia kuwa sekta ya gesi bado ni changa na inaendelea kukua taratibu na hadi sasa haijaweza kutumika kikamilifu nchini kutokana na gharama za kufunga mfumo wa kutumia gesi pamoja na uhaba wa vituo vya kujazia gesi.
Pia, soma=> Watumiaji wa gesi asilia kwenye magari wamefikiwa, wawekewa tozo ya 382 kwa kila kilo
===

Serikali imekubali mapendekezo ya wabunge ya kuondoa ushuru ya Sh382 kwenye gesi asilia inayotumika katika magari.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza amesema hayo leo Alhamisi Juni 27,2024 wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2024.
Tangu kuanza kwa mjadala ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25, wabunge wamekuwa wakilalamikia kuhusiana na kodi hiyo kuwa inarudisha nyuma jitihada za Watanzania kuingia katika matumizi ya gesi asilia ambayo inapatikana nchini.
Amesema kamati hiyo ilikubaliana na mapendekezo ya Serikali ya kuelekeza mapato ya ziada (windfall profit) kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Barabara.
Hata hivyo, Kamati haikukubaliana na uanzishwaji wa ushuru Sh382 kwa kila kilo ya gesi asilia inayotumika kwenye magari.
Amesema kamati imefikia uamuzi huo kwa kuzingatia kuwa sekta ya gesi bado ni changa na inaendelea kukua taratibu na hadi sasa haijaweza kutumika kikamilifu nchini kutokana na gharama za kufunga mfumo wa kutumia gesi pamoja na uhaba wa vituo vya kujazia gesi.
“Hivyo, Kamati iliishauri Serikali kuondoa pendekezo hili na Serikali iliridhia,” amesema.