Serikali ya Tanzania imesema imeongeza posho za madaktari anapoitwa nje ya saa za kazi, posho ya sare za wauguzi na ile ya kuchunguza maiti kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miaka mingi imepita tangu madaktari na wauguzi chini, kuomba ongezeko hilo.
Hayo yamesemwa leo Jumatano, Julai 31, 2024 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akitaja maazimio ya mkutano wa siku tatu wa rasilimali watu ulioandaliwa ndani ya Kumbukizi ya Hayati Benjamin William Mkapa uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Miongoni mwa maazimio ni pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi tutaendelea kufuata maelekezo yako Rais Samia Suluhu Hassan katika hili.
Tumeshaanza utekelezaji wa kuongeza 'OnCall allowance' za madaktari zilikuwa hazijaongezwa, posho ya sare ya wauguzi, posho ya kuchunguza maiti na nyingine kuanzia Julai hii na hili ulituelekeza," amesema.
Chanzo:Mwananchi