Serikali yapeleka huduma ya mabasi ya Mwendokasi Kibaha

Jana nilipita palekituo cha sheli Maili moja,nilimkuta dada wa mwendo kasi akiita abiria wanaotaka kwenda Kivukoni moja kwa moja. Kwa hiyo yapo ya kivukoni ila sina uhakika kwa yale ya Gerezani direct
 
Jana nilipita palekituo cha sheli Maili moja,nilimkuta dada wa mwendo kasi akiita abiria wanaotaka kwenda Kivukoni moja kwa moja. Kwa hiyo yapo ya kivukoni ila sina uhakika kwa yale ya Gerezani direct
Safi kabisa.. Nikitoka Msata kituo cha kwa kwanza maili moja
 
Hahahaaa, tushawazoea aisee.

Kuna siku konda alitaka kunidhulumu chenji yangu, nilianzisha timbwili timbwili mbona alisalimu na kunipatia chenji yangu
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Watu wa Kibaha mmeletewa MWENDOKASI afu hamsemi!

Pichani ni MWENDOKASI ikiwa kituo cha basi NJUWENI MAILI MOJA

Mama anaupiga Mwingi

Hakuna bus toka mbezi to kariakoo/posta mpaka ukashuke kimara uanze kupambania tena bus lingine

Huko kibaha wataweza kuwa na route mpaka city center?
 
wasisahau ruti ya kuingia Hospitali ya Mloganzila.
Wananchi ni wengi sana wanatoka maeneo mbalimbali kufuata huduma.
 
tangia lini mkuu, maana nilitokea k.koo kwenda kumuona mgonjwa Mloganzila ilinibidi nipande zaidi ya gari 3.
sijaona mwendo kasi.
kama wameanzisha ruti ya kwenda Hospitali ya Muhimbili Mloganzila basi ni jambo jema.
 
Ule ufalme wa coaster za Mlandizi unafikia tamati!
Na jinsi ambavyo huwa wanajidai wakiwa wanapakia abiria mbezi, sisi tunaoshukia karibu huwa wanatukataza kukalia siti.
Nimekwazana nao sana kuhusu hili, utakuta mpiga debe kawekwa mlangoni anamuuliza kila abiria anayepanda kituo anachoshukia, ukisema unashuka maili moja au Loliondo, hawakuruhusu kupanda.

Hiki kiburi kitakoma sasa kwa ujio mwendokasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…