Serikali yarekebisha MIHULA ya Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Download waraka huu wa serikali (WARAKA WA ELIMU NA. 5 WA MWAKA 2012 KUHUSU MAREKEBISHO YA MIHULA YA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU)
 

Attachments

Ahsante ndugu. Napata swali kidogo, je mabadiliko ya muda wa kufanya mtihani wa Kidato cha sita hautaathiri mihula ya Vyuo Vikuu?
Ikiwa kwa sasa wanafunzi wa kidato cha Sita wanahitimu mwezi Februari lakini ikifika mwezi wa Septemba TCU na HESLB, kwa kutumia takribani miezi nane hawajafanikiwa kuandaa vyuo na mikopo, itakuwaje watakapopewa miezi minne, (Juni mpaka September)?
 

ndugu yangu inakoelekea wanaktaka kuwakalisha wwahitimu mwaka mzima nyumbani na pia usisahau kuwa kuna chokochoko za kuanzisha JKT huenda huo muda wa mwaka mumoja wa kusubiri kwenda vyuoni vijana wakautumia JKT
 
Natumia simu nashindwa kuusoma,,,,mtuambie waraka unasema nin?????
 
KWA UFUPI:
A: RATIBA ZA MITIHANI
Kidato cha Nne - Nomemba Wiki ya 1 (badala ya Oktober Wiki ya 2).
Kidato cha Sita - Mei Wki ya 1 (badala ya Februari Wiki ya 2).
Ualimu Cheti na Stashahada - Mei Wiki ya 1 (hamna badiliko).

B: MIHULA YA MASOMO.
Kidato cha 1 - 4; hakuna mabadiliko kwa mihula yote miwili.
Kidato cha 5 na 6;
Muhula wa 1 - Julai Wiki ya 1 mpaka Desemba Wiki ya 1.
Muhula wa 2 - Januari Wiki ya 1 mpaka Juni Wiki ya 1.
Ualimu Cheti na Shahada - sawa na mihula ya Kidato cha 5 na 6.
Tanbihi: Wanafunzi wote watapumzika mwezi Juni na Desemba.
Waraka huu unaanza kutumika tarehe 01 Januari 2013
 
Sasa Ina maana tutaongeza ada kwa wale walioko form Six ? maanake shule zilikokotoa kiasi cha kuwaweka wanafunzi mpaka mwezi wa pili .
 
ndugu yangu inakoelekea wanaktaka kuwakalisha wwahitimu mwaka mzima nyumbani na pia usisahau kuwa kuna chokochoko za kuanzisha JKT huenda huo muda wa mwaka mumoja wa kusubiri kwenda vyuoni vijana wakautumia JKT


Nakubaliana na wewe hoja yako sounds like ina akili sana!! Nafikiri huo ndio mkakati...ina maana wanarudia enzi zile za zamani!! Yaani kila waziri akiingia anabadili system anavyotaka!!!

LAKINI NINA SWALI (la kizushi).. Huyu kamishna wa Elimu Jina lake (Prof. E. P. Bhalalusesa) mbona kama la kutoka kwa ''majirani zetu'' na sio humu ndani kwetu? kuna mwenye data zaidi?
 
Jirani zetu wa wapi? Huyu alikuwa Profesa pale UDSM na alikuwa Mkuu wa Kitivo (sasa Skuli) cha Elimu, ni mtanzania kama wewe
 
mambo mengine yanakera sana yaani tz baada ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma, kwanza tunamaliza shule tukiwa na umri mkubwa kupita wenzetu halafu bado tena tunaongeza muda wa kupoteza nyumbani...
Kidato cha Nne anafanya mtihani Nomemba halafu anakuja kuanza form 5 mwezi julai! miezi 9 nyumbani! kwa bahati mbaya akifeli mtihani itabidi aje arudie tena mtihani mwaka unaofuata kwahiyo jumla ameshapoteza miaka 2!
na mbaya zaidi jkt inarudishwa kwa form 6 sasa sijui hapo itakuwaje iwapo mfumo wa elimu ya juu hautarekebishwa. Ninachosikitika zaidi ni kurudia kumeza matapishi
 

Jina lisikusumbue maana mikapa ya wakoloni ilichorwa na kupita katikati ya koo na kabila bila kijalisha wewe unabaki TZ au Rwanda, Congo au burundi. Mfano Siame, Sinkala, Silungwe wapo Tanzania na zambia kwa sababu tu kabila lao lilitenganishwa na cha ajabu chief wao makao yake makuu yako tanzania wakati anaishi zambia
 
Mungai ndie aliyetibua mfumo wetu wa shule sasa naona wameamua kurudisha ule wa zamani
Naona ktk level ya wizara kuwe na vitu mtu anaweza badilisha vingine iwe kama amri kumi vile hakuna kubadilisha unless wadau wote wameshirikishwa espicially wananchi kupitia wabunge wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…