Serikali yarudisha Maonesho ya Wakulima "Nanenane", kitaifa mwaka 2021/2022 kufanyika Mbeya

Serikali yarudisha Maonesho ya Wakulima "Nanenane", kitaifa mwaka 2021/2022 kufanyika Mbeya

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Serikali ya awamu ya 6 kupitia Wizara ya Kilimo imerudisha upya Maonyesho ya Wakulima Nanenane baada ya kuzuiwa kufanyika kwa miaka kadhaa ya uongozi wa awamu ya 5.

Kwa mujibu wa Waziri Bashe, Serikali inakusudia kuyafanya maonesho hayo ya nane name kuwa maonesho rasmi ya Kimataifa ya Wakulima na Mazao yake hivyo kualika Mataifa mbalimbali na makampuni makubwa ya kilimo Duniani.

Kwa mwaka huu wa 2022,Maonyesho ya Wakulima Nanenane yatafanyika Kitaifa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwenye viwanja vya John Mwakangale, Uyole jijini Mbeya.

Niiombe Serikali itakapoyafanya kuwa ni Maonyesho rasmi ya biashara zinazohusiana na Kilimo,yawe yanafanyika Mkoa wa Mbeya badala ya kuyapeleka Dar au Mikoa mingine.

Hii ni kwa sababu Mkoa wa Mbeya unatambua Sijui ya Nanenane kama sikuu rasmi na watu huwa wanasherehekea Sana tuu kuliko maeneo mengi ya Nchi.

Kwa muktadha huo wakiyapeleka Mbeya basi yatapata umaarufu mkubwa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220531-131627.png
    Screenshot_20220531-131627.png
    169.3 KB · Views: 28
Kwa mkoa wa Mbeya nane nane ni zaidi ya Krismas,mwaka mpya au Idd.

VP mgeni rasmi kwenye ufunguzi 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220731-134257.png
    Screenshot_20220731-134257.png
    131.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom