Serikali yasema imewapa muda TUCTA wakajadiliane kuhusu mishahara mipya, na TUCTA wasema wameipa muda serikali

Serikali yasema imewapa muda TUCTA wakajadiliane kuhusu mishahara mipya, na TUCTA wasema wameipa muda serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema wameipa TUCTA muda wakajadiliane kuhusu mishahara mipya kisha walete mapendekezo yao serikalini.

Naye Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya amesema TUCTA wameipa muda Serikali ikaje na ufafanuzi juu mishahara kuwa pungufu ya Kima kilichoahidiwa.

Rais Nyamhokya amesema TUCTA ilitegemea ongezeko la 23.3% lingekwenda kwa bima vyote vya mishahara kama ilivyozoeleka katika miaka iliyopita.

Source ITV habari
 
Ina maana siku zote hizo walishindwa kuja na mapendekezo na maelezo?

Wanaona walimu watoto
 
Huku nako watumishi wanauliza hao TUCTA nani aliwatuma kuilalamikia serikali kuhusu mshahara
 
Mtumishi na akili zake anakatwa mshahara anachangia TUCTA
Hao tucta wanalalamika hivyo si kwamba wanamuonea huruma mtumishi ila wameona makusanyo ya ada kutoka kwa vyama vya wafanyakazi hayajaongezeka kwa kiwango walichotarajia
 
Rais wa TUCTA auambie umma wa Watanzania kilichokuwa kimekubaliwa ni kipi? Ili umma ujue Ukweli wa hili jambo hapa naona Dana Dana nyingi.
 
Na huo muda haijafika! Hilo 'TUTA' litajisahaulisha, na kukumbuka Mei Mosi, 2023.
Imetokea hiyo! Kila mtu ale urefu wa kamba yake.
Ingewezeksna tusio na kamba tungeomba hata kusaidia kubeba kamba za wengine.
 
Back
Top Bottom