Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya Mradi wa Umeme wa Kinyerezi One ambao pia itatumika katika Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR na kueleza kufurahishwa na maendeleo ya mradi huo, leo Jumatano Desemba 13, 2023.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Kamati ilifika eneo hilo kukamilisha ziara ambayo ilianzia Mkoani Morogoro kukagua miundombinu ya umeme ambayo inawezesha mradi wa Reli wa SGR.
Amesema Kamati hiyo imeshauri mambo kadhaa ikiwemo kuongeza na kuchagiza mambo yanayoweza kuboresha Uchumi wa Wananchi, mfano kuwekeza kwenye gesi inayotumika kwenye magari.
Daniel Sillo
“Tunafahamu kuna changamoto ya foleni kwa wenye magari wanaotumia nishati ya gesi, lakini uwekezaji ambao Serikali inafanya wa kuendelea kuboresha huduma ya nishati ya gesi ili uwe na mazingira rafiki zaidi.”
Ameongeza “Pia Kamati imetushauri taasisi ambazo zina watu zaidi ya 100 waendelee kufungiwa gesi kwenye taasisi zao, hilo tumelipokea na tutalifanyia kazi.”
Neno la KamatiAkizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo ambaye pia ni Mbunge wa Babati Vijijini amesema Watanzania wana hamu ya kuona safari za Reli ya SGR zinaanza, hivyo lengo la ziara yao ni kuona maendeleo na hatua zilipofikia.
Amesema “Kamati tumekuja kushuhudia kazi inayofanyika katika chanzo cha umeme unapozalishwa, tumeona Lot 1 (Awamu ya SGR) ya Dar es Salaam hadi Moro imekamilika kwa 100% ikitimua gharama ya Tsh. Bilioni 76.23, eneo linalofuata kutoka Morogoro hadi Dodoma kiasi kilichotumika ni Tsh. Bilioni 97.75 na imefikia 99%, tunaipongeza Serikali kwa hatua hii.”
Naibu Katibu Mkuu
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka amesema Wizara ya Nishati kupitia Shirikisha la Umeme Tanzania (TANESCO) imejiandaa kwa ajili ya Mradi wa SGR na ziara hiyo ambayo pia ilihusisha eneo la Msamvu (Morogoro) kabla ya kufika Kinyerezi inalenga kubaini maendeleo ya kazi zilipofikia.
Athumani Mbuttuka
Amesema “Kamati imeridhika na kazi ambayo imefanyika, ziara hii pia imetembelea GASCO ambao ni wasambazaji wa nishati ya gesi kwa ajili ya uzalishaji, wametoa maelekezo ambayo tumeyachukua.
“Wakati huohuo, tumewaelekeza mipango yetu kama Serikali ili kuongeza uzalishaji wa gesi.
“Aidha amesema kuwa Bwawa la Mwalimu Nyerere litakapoanza uzalishaji wa umeme Januari 2024 litaweza kupunguza matumizi ya gesi ambayo itahamishiwa kwenye matumivi ya viwandani.”
Pia, soma;
KERO - √ - Foleni ya kuweka gesi Dar kwenye magari ni tatizo
Mchangamoto tunaopitia wakati wa kujaza gesi kwenye magari ni kero kubwa ya foleni inayotokana na wingi wa wenye uhitaji huku sehemu za kujazia zikiwa chache. Hicho ni kikwazo kikubwa pia kwa madereva hasa wale ndugu zangu wa Taksi Mtandao kwa kuwa wanatumia muda mwingi kwenye foleni ya gesi...