Big up Kipanya. Saafi sana ujumbe umefika! Sijui kama riafande Mkuchika limeiona hii.
Nahofia isije ikatokea kesho tukasikia MASUOD KIPANYA AMEFUNGIWA KWA KUDHALILISHA SERIKALI YA JK KWA KUCHORA VIKARAGOSI VYENYE UCHOCHEZI WA KISIASA.
Naomba washauri wa Kikwete akiwemo Januari Makamba, Ridhiwani Kikwete na Mwandishi wake wa habari Salva Rweyemamu wampelee hii picha ya Kigaragosi cha Masoud wa Kipanya. Hapa ujumbe umefikaaa!!!
Hebu sikiliza hii video toka kwa Obama na mkewe Michelle wakizungumzia uchaguzi wa Marekani utakaofanyika hivi karibuni.
Obama na Michelle wanawaambia Wamarekani kuwa uamzi watakaoufanya siku ya kupiga kura ni kwa ajili ya mstakabali wa maisha yao ya baadaye na watoto wao.Listen and get the point.
Na sisi kama Watanzania tunatakiwa ifikapo 31.10.2010 kuchukua maamuzi ambayo yatakuwa kwa ajili ya Maisha yetu na watoto wetu kwa siku za usoni.