Serikali yasema treni ya SGR haitokuwa na tatizo la umeme

Sasa hivi yenyewe hapa nilipo umeme umekatika na kurudi ni saa 12 jioni na hii ni kila siku mwezi mzima sasa,sembuse huo mradi mkubwa ndio watauweza vipi.

Uongo mtupu.
 
Nalo litatuletea hasara kubwa zaidi ya yale madege.

Hakuna mradi wa Magufuli utakaoleta tija kwa walipa kodi. Waajirwa wa maahirika husika ndio wataonufaika kwa overtime na mishahara.
hii italeta faida mizigo ya kubeba ipo tofauti na biashara kichaa ya ndege ni hasara dunia nzima.
 
Hawajatatua matatizo ya huu unaokatika Mara kwa Mara, wanaongelea wa SGR. ?
Kwanza abiria watawapata wapi ilhali mabasi yanaboresha huduma?
Labda SGR ya Dar Mza abiria watakuwepo.
Waziri akae na ma engineer wake wa solve tatizo la umeme wa viwandani na majumbani kukatika Mara kwa Mara. Kama ma engineer hawana huo uwezo ruksa ku import toka Burundi
 
hii italeta faida mizigo ya kubeba ipo tofauti na biashara kichaa ya ndege ni hasara dunia nzima.
Kama watafungua inland container Depot pale Moro ili wazambia, warundi na watu wa Mwanza wachukulie makontena yao pale hii reli itakua na tija sana. Na foleni ya Kibaha Chalinze itapungua sana.
Hili wazo sijui Kama serikali yetu sikivu inalo...
 
Hamia huku Uzunguni
[emoji1][emoji1][emoji1] uwezo wangu unanilazimisha kuishi Moshono mkuu...uzunguni hapo pataniua...hakuna vibanda hata vya samaki wa mia mia wala hakuna vibanda vya mama mboga
 
Ngoja tusubiri tuone maneno mengi hatutaki
 
Umeme wa Tz huwa unakatika kwa dakika 10 tu!! Tutaona.
 
Labda kama baadhi ya mabehewa yatakua ni power bank
 
Hii nchi full comedy.
Walivyojenga hao watathmini hawakujua kuwa kuna bundi, kima n.k?
Kwanini hawakuweka mfumo wa kupambana nao bila kuathiri shughuli za usafiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…