serikali yatafuta watu waliosoma sayansi kuanzia 1998-2013 kuziba nafasi za ualimU

BINARY NO

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
2,151
Reaction score
2,162
Tangazo ambalo nimekumbana nalo leo ofisini ni kua kutokana na uhaba sugu wa walimu wa sayansi basi imekuja na mpango wa miezi mitatu wa kutrain watu waliosoma masomo yote ya sayansi na hesabu na awe ana ufaulu wa subsidiary results yani 'S' kwenye masomo mawili basi watapelekwa kusomea stashahada kwa miaka miwili....So ilo tangazo linataka watu wote walio tiyari kuanzia huo mwaka basi wajiunge haraka kuokoa jahazi ambalo linaelekea kuzama la uhaba sugu la walimu wa masomo ya science! na lazima wawe wamefika kidato cha 5 na 6
My Take! Je hili ndo litakua suluhisho la ufaulu mbovu wa masomo ya sayansi kwa kuchukua watu waliofeli kwani kwa ufaulu wa S kwa mtu aliesoma advance yani haukupeleki popote!
 

Hebu toa Suluhisho lako ili tuache hili.
 
ngoja tumsikie wazo lake maana watu wamezidi kubeza karibu kila kitu kinachofanywa na serikali wao ni kubeza tu

Ngoja tusubiri maana Watanzania siku hizi tunabeza tu bila kujua 'Some thing is better than nothing'.
 
Ni hatua nzuri kwa kweli hali ni mbaya huko mashuleni jamani.
 
wazo zuri kuna mtu wangu alipiga wani ya 13 akapata s mbili a level sidhani kama hatashindwa kufundisha physics ambayo alipata A katika pcm yote alikuwa na point nne
 
wazo zuri kuna mtu wangu alipiga wani ya 13 akapata s mbili a level sidhani kama hatashindwa kufundisha physics ambayo alipata A katika pcm yote alikuwa na point nne

mkuu one ya 13 mmh! ya o level au advance? mbn hyo ni 3 kwa advance!
 
Hebu toa Suluhisho lako ili tuache hili.

Ukienda vyuo vikuu vijana wanafanya ngono tu na wakati wa likizo hawana kitu cha kufanya...kwa nini wasichukuliwe hawa na kwenda kufundisha?Kuna wahitimu wa sayansi kutoka vyuo vyetu wanakaa mtaani kusubiri ajira n.k n.k
huwezi kuchukua failures wakafundishe halafu ukategemea ubora wa elimu.
Kuna wafanyakazi(walimu) wanazungukazunguka tu huko wizarani kwa nini wasipatiwe vipindi au topics za kufundisha?
Tusiwe na fikra mgando!
 

lipo moe juzi nilipita wizara ya elimu nililiona box la kukusanyia barua bridging course lipo upande wa kulia kama unaingia ndani lipo opposite na mbao ya matangazo
 
HAPA BILA KUBORESHA MASLAHI YA WALIMU,...MTAKUWA MNAPOTEZA WALIMU.2000 WALIOPO KAZINI NA KUINGIZA 100 WAPYA. RATE YA WALIMU KUBADILI FAN NI KUBWA KULIKO WANAOINGIA...aluta continua
 
Unajua wazo sio baya ila inabidi wajiulize kwa kufanya utafiti, ;
1. Kwanini uhaba huu umetokea?
2. Je hata hawa wanaongizwa kwenye hii program watakaa kufundisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…