Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
KWA UFUPI
Matukio ya kuua watu wenye ulemavu wa ngozi(albino0 yalishika kasi miaka minne iliyopita katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Mara. Baadaye yalianza kuhamia mikoa mingine jambo ambalo lilikuwa janga la kitaifa. Watu wengi walikamatwa, lakini hatua za wazi hazijajulikana.
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun (UTSS) ,Vicky Ntetema amesisitiza kuendelea kusubiri utekelezaji wa hukumu ya kunyongwa kwa wahukumiwa wote waliobainika kukutwa na makosa ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Tutaendelea kusubiri maana kwa sasa tunapozungumza na Serikali hutueleza kwamba baadhi ya wahukumiwa hao wamekutwa na makosa mengine ya mauaji hivyo tunasubiri hatua za mwisho,alisema Vicky.
Vicky alizungumza kauli hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Mwigulu Matonange (10) ambaye alikatwa mkono wake wa kushoto Februari 15, mwaka huu kijijini kwao Msia wilayani Sumbawanga huko Rukwa.
Vicky alisema mtoto huyo alifikishwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuendela na matibabu katika Taasisi ya Moi kutokana na ombi lake la kukataa kuendelea kuishi kijijini kwao.
Tumemhamisha kutoka Kituo cha Afya cha Mtowisa, alisema.
Kwa upande wake mtoto huyo alisema kwa sasa hatakuwa tayari tena kurudi kijijini kwao Msia kutokana na vitisho alivyovipata kutoka kwa watu hao. Sitaki kurudi kijiji,waliniambia wakiniona watanikata tena mkono na wataniuaalisema kwa lugha ya Kisukuma.
Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu wa ngoz i(albino) nchini Ernest Kimaya anasema tangu mwaka 2000 mpaka sasa takwimu zinaonyesha albino 35 wamejeruhiwa, makaburi 19 ya makaburi albino yalifukuliwa na watatu waliuawa mkoani Rukwa na Tabora.http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1720768/-/128lpun/-/index.html