Serikali yatangaza kushuka kwa bei za mafuta

Anna Nkya

Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
69
Reaction score
341
Serikali kupitia Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta.

Taarifa iliyotolewa leo na EWURA inaeleza kwamba, Ikilinganishwa na bei za mwezi Desema 2021, bei za Januari 2022 zitapungua kwa kati ya Shilingi 4 na 35 kwa lita ya petroli; na kati ya Shilingi 43 na 67 kwa lita ya dizeli isipokuwa kwa bandari ya Mtwara ambapo bei zitaongezeka kwa Shilingi 2 kwa lita; huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Shilingi 99 kwa lita.
.
Moja kati ya hatua muhimu zilizosababisha kushuka kwa bei hizo, ni kupunguzwa kwa tozo za taasisi za Serikali.

Vilevile, kutokana na kuendelea kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia, Serikali iliahirisha ukusanyaji wa ada ya mafuta (petroleum fee) kuanzia Desemba 2021 na hivyo kufanya bei ya juu kufikiwa katika mwaka 2021 kuwa ni Shilingi 2,510 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam, Shilingi 2,525 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Tanga na Shilingi 2,569 kwa lita ya petroli iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.

Bila ya kufanya maamuzi haya, bei za mafuta zingefikia kiwango cha juu cha Shilingi 2,638 kwa lita ya petroli (Dar es Salaam), Shilingi 2,648 kwa lita ya petroli (Tanga); na Shilingi 2,693 kwa lita ya petroli (Mtwara).

b429c787c8a6aa1cc5d5b788079cd5ea.jpg
 
Swali linabaki moja tu, Bulk procurement system imesaidia nini? Pia Mh. Makamba alitembelea nchi zinazozalisha mafuta duniani na kuzungumza nao possibilities za kuagiza moja kwa moja toka kwa wazalishaji wa mafuta. Je nini kimetokea kufuatia mazungumzo hayo?
 
Makamba hana jeuri ya ushawishi wa aina hio, alienda kuzurura kwa faida yake tu
 
Tunataka yashuke adi kufikia 1700. Hizo shilingi 2 hazina maana ni yale yale tuu. Hata kupunguza 100 ni yale yale tuuu hakuna wanachofanya.
 
Swali linabaki moja tu, Bulk procurement system imesaidia nini? Pia Mh. Makamba alitembelea nchi zinazozalisha mafuta duniani na kuzungumza nao possibilities za kuagiza moja kwa moja toka kwa wazalishaji wa mafuta. Je nini kimetokea kufuatia mazungumzo hayo?
Justification za kupiga perdiem tu hakuna impact ya hayo maziara
 
Serikali kupitia Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta.

Taarifa iliyotolewa leo na EWURA inaeleza kwamba, Ikilinganishwa na bei za mwezi Desema 2021, bei za Januari 2022 zitapungua kwa kati ya Shilingi 4 na 35 kwa lita ya petroli; na kati ya Shilingi 43 na 67 kwa lita ya dizeli isipokuwa kwa bandari ya Mtwara ambapo bei zitaongezeka kwa Shilingi 2 kwa lita; huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Shilingi 99 kwa lita.
Mtwara sio Tanzania ?

Hapo wangesema mabadiliko ya Bei na sio Kushuka kwa Bei...
 
Si mlisema Corona imesababisha kupanda bei,kwani imekwisha?
 
Haya wenye magari leo mmenunua mafuta lita 1 bei gani

Ova
 
Serikali inayotegemea kodi uumiza watu wake
 
Tunataka yashuke adi kufikia 1700. Hizo shilingi 2 hazina maana ni yale yale tuu. Hata kupunguza 100 ni yale yale tuuu hakuna wanachofanya.
Wanashusha shilling 2 mwezi huu,alafu mwezi ujao watapandisha shilling 4!!
 
Back
Top Bottom