Serikali yatenga Bilioni 4 kuimarisha miundombinu Jangwani

Serikali yatenga Bilioni 4 kuimarisha miundombinu Jangwani

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
Serikali kupitia Mfuko wa Barabara (Road fund) imesema ipo tayari kupitisha kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili ya kumlipa mkandarasi atakaepatikana ili kuboresha miundombinu ya Jangwani mara baada ya uhakiki wa makisio hayo kukamilika na kujiridhisha.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Bodi ya mfuko huo, Mwenyekiti wa Bodi Bw. Joseph Haule, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto hiyo haraka kabla ya mvua za masika kuanza.

"Bodi imeona tatizo hili na tumeliona kama suala la dharura, ndio maana tumekuja hapa kujionea hali halisi ili kutafuta njia sahihi ya kutatua tatizo hili ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu", amesema Mwenyekiti wa Bodi.

Aidha, Bw. Haule amefafanua kuwa kweli tatizo ni kubwa, mfereji una kina kifupi na makalvati mawili makubwa yaliyopo hapo yameziba kabisa.
Ameongeza kuwa nia ya Bodi ni kuona wananchi na wasafirishaji wanatumia muindombinu hiyo wakati wote wa mvua na kiangazi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake imeandaa mkakati wa muda mrefu kuhusu miundombinu hiyo ambapo amesema kuwa kwa sasa wataalamu wanafanya usanifu wa kina kwa ajili ya kuja na suluhisho la kudumu ikiwemo ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 300.

Mwakalinga amefafanua kuwa aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa haraka ikiwemo kutoa mchanga ambao umetuama katika eneo hilo ili kuinusuru miundombinu hiyo.

Naye, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ngusa, amethibitisha kuwa ofisi yake inaendelea kuhakikisha kuwa michanga inayotuama katika eneo hilo inatolewa kwa wakati ili kuruhusu magari kuweza kupita mara baada ya mvua kunyesha.

Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wametembelea eneo la Jangwani kujionea hali halisi ya miundombinu katika eneo hilo ambayo imekuwa ikiathiriwa na mvua na kusababisha kufunga mawasiliano ya watumiaji wa barabara ya Morogoro hususani eneo hilo kila mwaka.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Nchini (Road Fund) kiasi cha Tsh Bilioni 4 ambazo ni Mapato ya ndani zitatumika kujenga na kukarabati miundo mbinu ya eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Matumizi Sahihi ya Rasilimali zetu huleta Matokeo chanya kwetu sote.

Hongera sana Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kusimamia nidhamu kikamilifu.
 

Attachments

  • FB_IMG_16069859898357300.jpg
    FB_IMG_16069859898357300.jpg
    22.7 KB · Views: 2
  • FB_IMG_16069859862406228.jpg
    FB_IMG_16069859862406228.jpg
    19.6 KB · Views: 2
  • FB_IMG_16069859826318386.jpg
    FB_IMG_16069859826318386.jpg
    26.5 KB · Views: 2
  • FB_IMG_16069859786358798.jpg
    FB_IMG_16069859786358798.jpg
    13.1 KB · Views: 2
Mkuu ume attach hadi picha ya Ngurdoto Hostel ooh No Hotel nayo inahusika kukarabatiwa kwa mabilioni kama jangwani ama?
 
Bilioni nne hazitoshi hapo, hiyo barabara inyanyuliwe juu kuanzia fire mpaka mapipa mithili ya daraja.
 
Hela iliyotumika hapo mara ya kwanza imeisha, sasa kikoba kingine kufidia hela ya manunuzi ya watu.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Nchini (Road Fund) kiasi cha Tsh Bilioni 4 ambazo ni Mapato ya ndani zitatumika kujenga na kukarabati miundo mbinu ya eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam....
Jangwani bila flyover hakuna kitu
 
Bil4.??? Imalize tatizo .????

Labda wenzetu wanajua zaidi, ngoja tuone...
 
Bil4.??? Imalize tatizo .????

Labda wenzetu wanajua zaidi, ngoja tuone...
Soma vizuri. Hiyo ni short term plan; kufukua michanga, makaravati, nk

Suluhisho ni kuweka daraja refu la mita 300 ambalo kwa sasa linafanyiwa usanifu. Au umesoma kichwa cha habari tu ukaja fasta kukoment.
 
Soma vizuri. Hiyo ni short term plan; kufukua michanga, makaravati, nk

Suluhisho ni kuweka daraja refu la mita 300 ambalo kwa sasa linafanyiwa usanifu. Au umesoma kichwa cha habari tu ukaja fasta kukoment.
Hizi short plan zipo since when na zimesaidia nn.????
 
Back
Top Bottom