beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Serikali imetoa miezi mitatu kwa shirika la nyumba la taifa NHC kuwa limekamalisha miradi yote ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wananchi kwa gharama nafuu hatua ambayo itatoa nafasi kwa serikali kupitia shirika hilo kuendelea na miradi mingine ya nyumba katika kupunguza tatizo la makazi hapa nchini.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi, ametoa agizo hilo baada ya kutembelea nyumba 50 zinajengwa na shirika hilo eneo la Buhare katika manispaa ya Musoma, ambapo amesema kuwa kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati, kunachangia kuliingizia shirika hilo katika gharama kubwa za ujenzi.
Hata hivyo waziri huyo ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, amelitaka hilo la nyumba la nyumba la taifa kufikiria sasa kupuunguza gharama za uuzaji wa nyumba hizo, kwani amesema wananchi wengi wa kipato cha chini wameshindwa kumudu ghama za ununuzi wa nyumba zake kutokana na ukubwa wa gharama hizo.
Naye meneja wa NHC mkoa wa Mara Bw Frank Mambo, amemueleza waziri huyo kuwa ujenzi wa nyumba hizo upo katika hatua za mwisho, huku akiwaomba wananchi na taasisi za serikali kujitokeza sasa kununua nyumba hizo za kisasa.