Serikali yatoa siku 14 kwa Bodi ya Nafaka kukamilisha malipo ya Wakulima wa Korosho

Serikali yatoa siku 14 kwa Bodi ya Nafaka kukamilisha malipo ya Wakulima wa Korosho

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko Dkt Anslem Moshi kukamilisha malipo ya wakulima wote waliouza korosho msimu wa mwaka 2018/2019.

Waziri Hasunga ametoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua shughuli za utendaji kazi zinazofanywa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Jijini Arusha.

Amesema kuwa Bodi hiyo ilipewa dhamana la kununua korosho mwaka 2018 kwa niaba ya serikali na tayari serikali imeshatoa fedha zote kwa ajili ya wakulima lakini bado CPB haijakamilisha malipo hivyo ni lazima malipo yakamilike ndani ya siku hizo.

“Ndani ya siku 14 sitaki kusikia malalamiko ya wakulima lazima wakulima wote wawe wamelipwa fedha zao haraka iwezekanavyo” Alisisitiza

Katika ziara hiyo pia Waziri Hasunga amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko kuwasilisha haraka mpango kazi wa namna viwanda hivyo vitakavyofanya kazi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zitakazohitajika na wateja na kukidhi matarajio ya serikali ikiwa ni pamoja na kuainisha idadi ya watumishi wanaohitajika.

Hasunga ameiagiza kampuni ya Monaban ambayo ilikuwa imekodisha kiwanda hicho kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa mwaka jana ya kuhamisha mali zao zote zilizopo katika eneo hilo la serikali kwani kesi mahakamani na notisi ilishaisha.

Akiwa kiwandani hapo Waziri Hasunga amebaini uchakavu wa mitambo iliyopo pamoja na uchache wa watumishi wanaofanya kazi katika kiwanda hicho hivyo ameagiza kufanyika ukarabati wa majengo hayo kuanzia mwezi Agosti badala ya Octoba kwa taasisi hiyo ilivyopanga.

“Tukisubiri mpaka mwezi wa kumi tutakuwa tumechelewa kwa kuwa mvua zitaanza kunyesha jambo ambalo litapelekea kushindikana kufanyika ukarabati” Amesema

Amesema kuwa Lengo la serikali ni kufufua viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao ya nafaka nchini ili kuzalisha bidhaa mbalimbali kama unga N,k na kuuza katika masoko ya ushindani ndani na nje ya nchi.
 
Wameshajua kwamba siku za kampeni zimekaribia. Yaani korosho za mwaka juzi, leo ndo amekumbuka kutoa siku 14 kwa bodi ya mazao mchanganyiko?

Jamaa ni matapeli sijapata kuona.
Yani serikali ya kitapeli kabisa hii.
 
Yani hili zao mngejua ugumu wanaopata wakulima ilitakiwa wawalipe kwa wakati maana miche unahudumia mwaka mzima alafu pesa zinakaa mpaka unasahau dahh mkulima sijui atatoa lini aisee maana pesa anaipata yote ananunua pembejeo tena kazi yake inakua kunufaisha wanunuzi tu
 
Wameshajua kwamba siku za kampeni zimekaribia. Yaani korosho za mwaka juzi, leo ndo amekumbuka kutoa siku 14 kwa bodi ya mazao mchanganyiko?

Jamaa ni matapeli sijapata kuona.
Korosho ni mzimu unao tisha machoni pa serikali hii.
Kiukweli ilichemka sana namna ilivyo ingilia biashara ya zao la korosho.
Naamini kuna kitu wamejifunza wenye dhamana.

Fitina za wenye viwanda vya sukari nchini wameiingiza chaka serikali kwenye suala la sukari pia. Imekuwa rahisi kuingia chaka sababu ya tamaa njema ya kuimarisha mpango wa Tanzania ya viwanda. Hili nbalo ni somo lingine kwa serikali.
 
Na miwaziri nayo inapoingia huko inakuwa kama mitaahira fulani hivi! Yaani kama fedha ilishatoka bodi ilikuwa inamsubiri nani kuwalipa wakulima? Yaani Magu atoe hela halafu uikalie utabaki kweli? Hapo Hasunga asituone sisi wajinga! Tukutane Oktoba kwenye sanduku!
 
Kazi ya serikali ni kukusanya Kodi,kuweka mazingira ili wananchi wafaidike kwa mazao yao sasa zao la korosho limekufa kifo cha mende baada ya magufuli kutangaza atanunua yeye huku akitumia mitutu ya jeshi kukusanya na kuiba korosho hizo ,muulizeni huyo magufuli aliwahi kuuza hata maji ya kandoro
 
Back
Top Bottom