The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Serikali imewapa siku tatu wawekezaji wote wa kigeni kuondoka katika maeneo ya mgodi wa madini Nditi uliopo wilayani Nachingwea mkoani Lindi na kuwaacha wachimbiji wadogo katika eneo hilo kwani ni eneo la rashi.
akizungumza mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo akiwa ameambatana na kamati ya usalama wilaya amesema kuwa maelekezo ya serikali lazima yazingatiwe kwa kuwaondoa wageni wote wasio kuwa raia wa Tanzania katika maeneo ya mgodi paka pale serikali itakapotoa maelekezo mengine huku wakitakiwa kutoendelea na shughuli yoyote ya uchimbaji wala kusafirisha kitu kutoka mgodini kwani eneo hilo ni maalumu kwa wachimbaji wadogo.
aidha ameongeza kwa kusema kuwa wanaweza kuishi karibu na maeneo hayo au katika wilaya hiyo ya Nachingwea lakini sio katika mgodi huo paka pale serikali itakapotoa tamko.
kwa upande wake mwandisi Emanuel Shija ambae ni afisa madini mkoa Lindi ameeleza kuwa maeneo yote ya uchimbaji wanatakiwa kuwepo watanzania na kama watahitaji usaidizi wa kitaalamu kutoka kwa mtu wa nje ni lazima wafuate utaratibu wa kukata kibali kitu ambacho akijafuatwa katika eneo hilo.
aidha ameongeza kuwa wengi wao walikata leseni ya ununuzi wa madini na baadae wakajiingiza katika uchimbaji kinyume na utaratibu.