Serikali yatoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Mpox

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TISHIO LA UGONJWA WA MPOX​

Agosti 17, 2024, Dodoma.

Ndugu wananchi, Itakumbukwa kwamba, Wizara ya Afya ilitoa tadhadhari kwa umma kuhusu ugonjwa wa Mpox mnamo tarehe 3 Agosti 2024. Katika kipindi chote, Wizara imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huu duniani. Aidha, tarehe 14 Agosti 2024 Shirika la Afya Duniani lilitangaza ugonjwa wa Mpox kuwa ni Dharura ya Afya Kimataifa.

Ndugu wananchi, Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa Mpox umeendelea kutolewa taarifa kutoka nchi mbalimbali duniani, ambapo hadi June 2024, jumla ya wagonjwa 99,176 na vifo 208(0.2%) vimethibitishwa. Aidha, taarifa zinaonyesha kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huu katika baadhi ya mataifa jirani na nchi yetu na hivyo kupelekea kuhitajika hatua za tahadhari kwa kila Mtanzania kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini.

Pia soma: WHO: Mlipuko wa Ugonjwa wa Mpox ni janga la Kiafya la Kimataifa

Ndugu wananchi, Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuzuia kuingia nchini ugonjwa wa Mpox na kuimarisha utayari wa kukabiliana nao. Hii ni pamoja na kuandaa na kusambaza vipeperushi vya elimu ya jamii kuhusu dalili na njia za kujikinga na ugonjwa wa Mpox. Vilevile, wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika ngazi zote; kuandaa miongozo ya tiba na kinga kwa watumishi; pamoja na kuimarisha uwezo wa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ili kuweza kupima sampuli za wahisiwa wa ugonjwa wa Mpox.

Ndugu wananchi, Mpaka sasa, hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitika kuwa na maambukizi ya Mpox na nchi yetu ni salama. Hata hivyo, tunahitaji kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huu kwa kutekeleza yafuatayo;

i. Kutoa taarifa kwa kupiga namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu mwenye dalili za Mpox.

ii. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili au ngozi ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.

iii. Kuepuka kugusana, kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kumbusu mtu mwenye dalili za Mpox.

iv. Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono mara kwa mara.

v. Kuepuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.

vi. Safisha na kutakasa vyombo pamoja na matandiko yaliyotumika na mtu mwenye dalili za Mpox pamoja na maeneo yote yanayoguswa mara kwa mara kwa kutumia sabuni, maji na dawa za kutakasa za klorini mfano JIK.

vii. Vaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Mpox.

viii. Kuwahi katika vituo vya huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Mpox.

Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu ugonjwa wa Mpox na kuchukua hatua stahiki kuzuia ugonjwa huu kuingia nchini. Vile vile, tumeimarisha vituo vya huduma, maabara na upatikanaji wa dawa, vifaa kinga na tiba ili kutoa huduma stahiki endapo utaingia nchini.

Imetolewa na:
Prof. Tumaini J. Nagu
MGANGA MKUU WA SERIKALI

mpoxxx.jpg

mpoxx.jpg
 
View attachment 3073227
View attachment 3073226
Mbona sasa tangazo lake halijaambatana na vipeperushi vya elimu kuhusu ugonjwa wenyewe??
 
CovaX,,,MpoX,,,Mtandao X,,,Space X,,Tulieachana ni Wangu X....n.k
 
Back
Top Bottom