Serikali yatoa ufafanuzi madai ya Uwanja wa Mkapa kutia aibu kwa uchafu

Serikali yatoa ufafanuzi madai ya Uwanja wa Mkapa kutia aibu kwa uchafu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Uwanja.jpg

Nyasiii.JPG

Uwanja wa Mkapa kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Al Hilal, Februari 5, 2023.
Pia soma: Uwanja wa Mkapa unatia aibu, nani awajibike?
 
Baada ya kusoma mapendekezo ya wizara, nimegundua utetezi walioutoa mwanzo kwamba picha zilizotumika kuonesha uchafu zilipigwa mwaka 2020 hauna maana, wamekwepa tatizo tu.

Ambalo mbeleni wamekubali lipo ndio maana wamekuja na mapendekezo manne ili kuondokana na hali ya uchafu, na isiwe uwanja wa taifa pekee, bali viwanja vyote vinavyomilikiwa na CCM nchi nzima.
 
Yani ni aibu ukisoma hii barua na ukiangalia mechi zinazo chezwa kila uchwao ktk uwanja mbovu(sehemu ya kuchezea)

Wame shindwa kuchukua hatua stahiki kuokoa ata hiki kidogo tulicho bakiza

Wakicheza uwanja sehemu ya kucheza utageuka vumbi (kipara)
 
Uwanja wa mpira wa miguu una geuzwa uwanja wa disco, uwanja wa ibada, uwanja wa ngumu, uwanja wa kila kitu

Uwanja utumike kwa matumizi kusudiwa na sio kila matumizi wakati sio lengo haswa la ujenzi wenyewe
 
Majibu sijayaelewa, huyo mzabuni hadi kwenye pitch ya kuchezea au yeye ni masuala ya usafi wa uwanja tu, maana hadi leo naona hizo nyasi bandia zimechoka balaa, au mzabuni hajapaona au TFF au bodi ya ligi au sirikali yenyewe tu?
 
Ni lini serikali ya CCM ikakiri kosa? Kazi Yao ni kukanusha hata vitu ambavyo viko Wazi Kwa Kila Mtu.
 
Majibu sijayaelewa, huyo mzabuni hadi kwenye pitch ya kuchezea au yeye ni masuala ya usafi wa uwanja tu, maana hadi leo naona hizo nyasi bandia zimechoka balaa, au mzabuni hajapaona au TFF au bodi ya ligi au sirikali yenyewe tu?
Mkapa Stadium iko na nyasi bandia!!!???
 
Uwanja wa mpira wa miguu una geuzwa uwanja wa disco, uwanja wa ibada, uwanja wa ngumu, uwanja wa kila kitu

Uwanja utumike kwa matumizi kusudiwa na sio kila matumizi wakati sio lengo haswa la ujenzi wenyewe
Ndiyo sera za chama chako cha ccm hizo za kutengeneza mazingira ya hayo makongamano na matakataka mengine kufanyika humo uwanjani. Hivyo hutakiwi kulalamika.
 
Picha ya 2020??

Hapo kama kawaida lawama wanamptupia Magufuli.

Yaani awamu hii ni kujivua wajibu na kumtupia lawama Magufuli.
 
Pls kama kuna mwenye uhakika wa jibu hili anijibu, hivi uwanja huu una GROUNDMAN,huyu ni mtumishi muhimu mno kwenye utunzaji wa viwanja vyote vya michezo, je uwanja huu unaye mtu wa aina hii?
 
Huu uwanja haupo tayari kwa kashkashi za michuano inayokuja.

Yanga na Simba zote zina mzuka wa mashindano ya CAF yaliyo mbele yao, muonekano wa huu uwanja unaharibu vibe kabisa. Kwenye mechi ya Simba na Coastal Union, wachezaji wa Simba walikuwa wanastruggle sana kucontrol mpira na walikuwa wanaanguka sana wenyewe nadhani waliumwagilia maji kabla tu ya mchezo ili uonekane wa kijani zaidi.
 
Ulijengwa chini ya viwango.

HAKUNA HATA GEISER.
Bomba za kumwagilia Maji.

Tv MATANGAZO.

UWANJA UNATWAMISHA MAJI.

RANGI ZIMECHOKA.

HAKUNA MATUNZO
 
Ulijengwa chini ya viwango.

HAKUNA HATA GEISER.
Bomba za kumwagilia Maji.

Tv MATANGAZO.

UWANJA UNATWAMISHA MAJI.

RANGI ZIMECHOKA.

HAKUNA MATUNZO
Huu uwanja nadhani ujenzi wake uliishia njiani. Una dalili zote kuwa kuna mambo yalikatwa au kufanywa chini ya viwango, ndani na nje ya pitch.
 
Uwanja wa mpira wa miguu una geuzwa uwanja wa disco, uwanja wa ibada, uwanja wa ngumu, uwanja wa kila kitu

Uwanja utumike kwa matumizi kusudiwa na sio kila matumizi wakati sio lengo haswa la ujenzi wenyewe
Ule ni uwanja wa michezo na siyo uwanja wa mpira wa miguu tu,ndiyo maana lanes za riadha,uwanja wa kikapu na mpira wa Pete,we ulishaona lanes za riadha old Trafford au Emirates!?..vile ndiyo viwanja vya mpira
 
Uwanja wa mpira wa miguu una geuzwa uwanja wa disco, uwanja wa ibada, uwanja wa ngumu, uwanja wa kila kitu

Uwanja utumike kwa matumizi kusudiwa na sio kila matumizi wakati sio lengo haswa la ujenzi wenyewe
mapato,,mapato,,mapato,serikali inawaza mapato tu aiangalii changamoto zingine.
Mwamposa akikodi uwanja kwa mlioni 200 au zaidi serikali inachukua huku uwanja unapauka mpaka aibu.
 
Majibu sijayaelewa, huyo mzabuni hadi kwenye pitch ya kuchezea au yeye ni masuala ya usafi wa uwanja tu, maana hadi leo naona hizo nyasi bandia zimechoka balaa, au mzabuni hajapaona au TFF au bodi ya ligi au sirikali yenyewe tu?
Hakuna nyasi bandia kwa mkapa jiridhishe kwanza mkuu,bandia ziko Uhuru
 
Back
Top Bottom