Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Serikali yaunda tume ya vyuo vikuu
Itachunguza utata wa mikopo ya wanafunzi
na Happiness Mtweve, Dodoma
RAIS Jakaya Kikwete ameunda tume ya wataalamu 11, kufanya mapitio ya mfumo wa uendeshaji wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kuundwa kwa tume hiyo kulitangazwa jana mjini hapa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
Waziri Mkuu alisema lengo la tume hiyo ni kutaka kuimarisha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini.
Alieleza kuwa tume hiyo itafanya kazi kwa miezi miwili kuanzia Febeuari 14 mwaka huu na itatakiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi Aprili 15.
Alisema tume hiyo itaongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Profesa Makenya Maboko.
Wajumbe ni Masoud Mohamed Haji ambaye ni Ofisa Mahusiano wa Kimataifa, Dk. Eliawony Kristosia Meena, mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu cha Tumaini Arusha na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Zanzibar.
Wengine ni Paul Daniel Magwiza, Naibu Katibu Tume ya vyuo vikuu, Sarah Baharamoka, Mkurugenzi Msaidizi Uandishi Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Penina Mlama, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa tawi la Tanzania la taasisi inayopigania elimu kwa wanawake.
Pinda aliwataja wajumbe wengine wa tume hiyo kuwa ni Deo Mbasa Daud ambaye ni ofisa taaluma wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Kassim Almasi Umba, ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro na Anderson Mlabwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mikopo Benki ya CRDB.
Wengine ni ni Profesa Wilbert Abel Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Rosemary Rulabuka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Alieleza kuwa tume hiyo itateua Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwa wajumbe ambapo Sekretarieti ya Tume hiyo itatokana na wajumbe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)na Ikulu.
Alifafanua kuwa hadidu za rejea za tume ni pamoja na kuchambua kwa kina sheria namba tisa ya mwaka 2004 iliyounda Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kanuni zake ili kubainisha vifungu vinavyohitaji marekebisho kulingana na hali halisi ya utoaji wa mikopo.
Alisema hadidu nyingine za rejea ni kuangalia upya vigezo na sifa zinazozingatiwa katika utoaji wa mkopo endapo vinakidhi haja na mahitaji halisi ya waombaji na taifa kulingana na makusudio ya kuundwa kwa bodi.
Nyingine ni kuangalia kwa kina muundo wa bodi na ufanisi wake katika utoaji na urejeshwaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa mapendekezo na kuchunguza kiini cha malalamiko na mahusiano yasiyoridhisha kati ya bodi na wanafunzi, bodi na Taasisi ya Elimu ya Juu na kati ya bodi na Wizara ya Elimu na kutoa mapendekezo ya namna ya kurejesha mahusiano mazuri.