Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya imetoa dawa za kingatiba ili kudhibiti na kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele, ambapo watu 257,358 kati ya 265,217 walipatiwa kingatiba kwa mwaka 2024.
Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, amesema hayo Dar es Salaam Alhamisi Januari 30, 2025, wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani, yenye kaulimbiu "Tuungane. Tuchukue hatua. Tutokomeze Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele."
Kwa upande wa ugonjwa wa usubi, Waziri Mhagama amesema kuwa zaidi ya watu milioni 5.4 kati ya milioni 6.4 kutoka halmashauri 24 walipatiwa kingatiba, sawa na asilimia 85 ya walengwa.
Aidha, kingatiba dhidi ya trakoma ilitolewa kwa watu milioni 1.6 kati ya milioni 1.9 kutoka halmashauri saba, huku watoto milioni 8.6 kati ya milioni 9.8 wakipatiwa dawa za minyoo ya tumbo, ikiwa ni asilimia 88 ya walengwa.
Waziri Mhagama amesisitiza kuwa jitihada hizi ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha kuwa magonjwa haya yanatokomezwa kabisa nchini.