benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Kampuni ya Tembo Nickel imelipa zaidi ya Shilingi Bilioni 6.7 mwaka jana ikiwa ni kodi ya leseni za kuendesha kampuni hiyo.
Meneja Mkuu wa Tembo Nickel, Manny Ramos amesema kampuni hiyo pia ilitumia zaidi ya Sh bilioni 18.5 katika manunuzi ya vifaa na bidhaa mbalimbali. Kati ya kiasi hicho, Sh milioni 767 zilitumika wilayani Ngara pekee.
Alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi miradi kwa serikali ikihusisha sekta za afya na elimu na kutekelezwa kwa ufadhili wa Tembo Nickel kwa gharama ya Sh milioni 208.1.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa wodi ya kujifungulia katika Kata ya Bugarama, madarasa 11 na viti 160.
Kadhalika wahudumu wa afya ya msingi 18 walipewa mafunzo na baadaye wakapatiwa baiskeli 18 ili ku-wawezesha kuwafikia walengwa.
Ramos alisema watumishi wa ajira za kudumu 102 waliajiriwa na kampuni hiyo wakiwemo Watanzania 89 na kuwa Wazabuni 54 kutoka Halmashauri ya Ngara walipewa zabuni kusambaza vyakula na mahitaji mengine kwa kampuni hiyo.
Julai 8 mwaka jana kampuni ya Tembo Nickel ilisaini makubaliano na Halmashauri ya Ngara kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
Miradi hiyo ni katika sekta za elimu na afya inatekelez-wa katika kata za Bugarama, Bukiriro, Muganza, Rulenge, Mbuba na Keza, wilayani Ngara. Miradi 11 imetekelezwa na ilikabidhiwa kwa serikali.
Kati ya miradi hiyo, miradi saba inahusu sekta ya elimu ikihusisha ujenzi na ukarababti wa miundombinu ya madarasa na ofisi za walimu pamoja na madawati.Katika sekta ya Afya miradi mitatu imetekelezwa