Serikali yawaachia wananchi kuhusu mafuta ya ubuyu “kutumia ama kuacha

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Dar es Salaam. Serikali imesema suala la matumizi ya mafuta ya ubuyu sasa inawaachiwa wananchi wenyewe kutumia ama kuacha.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alisema hayo jana alipotoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa mafunzo ya wataalamu kutoka vitengo vya mbalimbali vya Udhibiti Dawa na Chakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu kutoka nchi 16 za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kwa kipindi cha mwezi sasa, watu mbalimbali kupitia vyombo wamekuwa wakitoa maoni ya kupinga kauli za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwamba mafuta hayo yana madhara kwa binadamu.
Dk Rashid alisema suala la mafuta ya ubuyu ni kwamba mlaji anapaswa kuwa na tahadhari hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuzuia vitu ambavyo vina madhara na vinavyoweza kusababisha athari kama saratani na magonjwa mengine.
“Mafuta ya ubuyu yana athari kama vitu vingine vyote vinavyokuwa na madhara kwa binadamu ila watu wanapaswa kujua kuwa madhara haya ni sawa na madhara ya mtu anayevuta sigara, licha ya tahadhari kuwekwa kuwa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya hivyo hivyo hata kwa mtumiaji wa mafuta ya ubuyu madhara yapo na yameshadhibitishwa na TFDA hivyo ni jukumu la jamii kuzuia tatizo hilo” alisema Dk Rashid.
Jana hiyo gazeti moja linalochapishwa kila siku liliwanukuu watalaamu wa Hospitali ya Ocean maarufu kwa kutibu saratani kwamba hawajaona kansa inayoweza kutajwa kwamba ilisababishwa na mafuta ya ubuyu.
Lakini Naibu Waziri alisisitiza kwamba licha ya kuwapo kwa taarifa kuwa mafuta hayo hayana madhara, lakini TFDA wamepima na kugundua madhara kwa mtumiaji, hivyo jukumu hili ni la kila mmoja kuhakikisha kuwa anaacha kutumia mafuta hayo au anaendelea.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, kusema kuwa mafuta ya ubuyu hayana madhara yoyote katika mwili wa binadamu kama yakitumiwa vizuri.

MCL
 
Mbona hawa wanatuchangaya akili zetu tumuamini kiongozi gani kati hao watu 3 ,

(1)Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. Anasema Serikali imawaachia Wananchi wenyewe kutumia Mafuta ya

Ubuyu kwa hiyari yao watumie au wasitumie.

(2)
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wanasema Mafuta ya Ubuyu yana madhara ukiyanywa yanaweza

kukuletea Magonjwa ya Saratani.

(3) Na
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, kusema kuwa mafuta ya ubuyu hayana madhara yoyote katika

mwili wa binadamu kama yakitumiwa vizuri.Haya tushike lipi kati ya hayo Maelezo ya Watu 3 tofauti?

ahhhh hii nchi yetu kweli inaongozwa hivyo hivyo tu bora liende kifo cha wengi ni harusi.

Kwa Ushauri

wangu
bora hayo Mafuta ya Ubuyu yangelipelekwa nje ya nchi kuchunguzwa je haya Mafuta ya Ubuyu yakiwa yanatumika kwa

kuyanywa je yanaweza kuleta Madhara kwa binadamu au hapana?Kisha ikipatikana majibu kuwa yanaleta madhara kwa binadamu kwa kuyanywa ndipo Serikali yetu iyapige marufuku kuyatumia huo ndio ushauri wangu .
 
Miaka mingi Wagogo wamekuwa wakila na kutafuna mbegu za ubuyu(mafuta ya ubuyu) hatujasikia madhara kwao, ukienda Ugogoni kuna wazee wanafika miaka mia ya kuishi ... Nadbani shida ya haya mafuta yanapandisha cd4s hivi biashara ya arv inatishiwa...napata picha sasa ni kwanini wanaodai kugundua dawa ya ukimwi wanapuuzwa,kusimangwa na vyombo ambavyo vingewapokea na kuanzisha tafiti za kina..
 
Hayo ndio madhara ya 'VITA YA MASLAHI' miongoni mwa 'wadau wa taasis za afya'
 
Hapa ndio inabidi nikumbuke yale maneno ya 'Enzi za Mwarimu' kuwa UBEPARI NI UNYAMA,yaani watu wanaangalia maslahi zaidi kuliko afya!nakubaliana na wewe 100% MORIA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…