#COVID19 Serikali yawaonya wanaojipatia vyeti feki vya chanjo ya Corona

Wizara ya afya ni wazembe, watu wanataka vyeti ili waendelee na safari zao, wao wanapiga porojo tu hadi sasa vyeti bado, hizi ndio mambo ambazo Magu alikuwa lazima apige watu chini ili akili zije.
wazembe sana
 
Vyeti vya nini? Yaani serikali iliyo na wataalamu wa IT imeshindwa kutengeneza data base inayoonyesha Name, ID/Paassport ukifanya scan kwa simu yako basi inaonyesha "Inoculated" very simple. Hivi tupo wajima kiasi gani hii nchi??
Chama Cha Mbumbumbu idiots party
 
Ndugu yangu ,swala la vyeti vya kuchanjwa corona' kwa jinsi hali ilivyo na tunavyoelekea duniani, kwa watu wanaotarajia kusafiri kwenda nchi yoyote nje ya Tz, cheti kitakuwa na umuhimu na wala hautaweza kuvuka bila document kama hizo, unless wewe ni mtu ambaye maisha yako yote itabidi ubakie nchini kwako.
Vyeti vya korona vinasaidia nini ama vina faida gani?

Vinazuia mtu kufa kwa corona ama?
 
Vyeti vya nini? Yaani serikali iliyo na wataalamu wa IT imeshindwa kutengeneza data base inayoonyesha Name, ID/Paassport ukifanya scan kwa simu yako basi inaonyesha "Inoculated" very simple. Hivi tupo wajima kiasi gani hii nchi??
Hii ipo USA, Philippines, na sehemu kibao lakini still Access to database ipo na kazi inafinyika na watu wanapewa utambulisho kama wa yule alie chanjwa. Huduma inapatikana kwa $200 tu.
 
Umenikumbusha kaka yake Mh. Medard Kalemani alikuwa mtendaji wa Kata wilaya ya chato akakutwa na vyeti feki🤣
 
Vyeti vya korona vinasaidia nini ama vina faida gani?

Vinazuia mtu kufa kwa corona ama?
Itafikia muda hutaweza kuingia nchi au hata ofisi fulani bila uthibitisho wa chanjo, sasa wasiotaka kuchanja itabidi watafute njia ya kuwa na huo uthibitisho.
 
Leo umeipinga serikali.

Watu watachanjwa sababu ya huduma tu,na sio kwa ajiri ya corona.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
Mkuu usijadanganye watu kibao wanaenda kwa hiari kuchanja.Ingekuwa chanjo imekosa wateja wangekuwa wanachanja Kila mtu,lakini ukienda Kama huna vigezo huchanji
 

Upuuzi mkubwa.
Kuzaliwa cheti
Kubatizwa cheti
Sd7 chati
4m4 cheti
4m6 cheti
Chuo cheti
Ndoa cheti
Corona cheti.

Imekuwa Nchi ya vyeti?
 
Hakuna cheti halali cha chanjo kilichowahi kutolewa baada ya kupima, ni usanii mtupu. Wanafanya hivyo huku wakiujua ukweli na siri iliyo nyuma ya chanjo
 
Haya matukio ndani ya michakato yote yenye kuambatana na wizi, kugushi ubabaishaji na vitu batili ndiyo haswa kinaonyesha taswira halisi ya CCM jinsi ambavyo kinaendesha shughuli za kiserikali. Motisha kubwa kuwa ni wizi na kujali matumbo yao.

Kama katika mambo muhimu tu ya kitaifa kama vile uchaguzi mkuu na ule wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji walithubutu kufanya wizi na hujuma pasipo kuwa aibu yoyote ile, Je! Nini ambacho kitawashinda kuendelea kufanya madudu yao tena?

Kama tu vyeti vya kitaaluma ama wasifu wa makada wa wengi umejaa mambo ya uongo na kugushi, Je! Wanashindwa ni kuwa na vyeti vya kugushi katika hili la chanjo za UVIKO 19?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…