PreGE2025 Serikali yawaonya wanaotaka kufanya fujo uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Serikali ya Tanzania imewaonya watu waliojipanga kuleta fujo, kujihusisha na rushwa ama kuleta sitofahamu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuwa ipo macho na haitatoa mwanya wa kufanyika hila hizo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 9, 2025 wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mwera (CCM), Zahoro Mohamed Ally.

Mbunge huyo amehoji Serikali imejipangaje kupambana na rushwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2025 ukizingatia kuna upungufu wa watumishi na vitendea kazi.

Akijibu swali hilo, Simbachawene amesema Serikali imejipanga na kudhamiria kuwa na uchaguzi wa huru na wa haki ambao viongozi watachagua kwa uwezo wao wa kuongoza na kuwahudumia wananchi, na sio kwa kuwarubuni wapiga kura kwa rushwa.

Your browser is not able to display this video.
 
Serikali ya CCM iandae Majela ya kufunga Watanzania milioni 60 watakaokamatwa lwa kugimbania HAKI zao za Kikatiba.
 
Kumbe uchaguzi upo palepale
 
Kuna mawaziri hawasikiki kabisa awamu hii, kama huyu baba
 
Serikali ikemee wizi wa kura inaoufanya kila uchaguzi , serikali hiyo nina uhakika haiwezi kukemea maana haiwezi kujikemea sababu ndio njia pekee ya kushinda uchaguzi ikitumia vyombo vya dola.

Hakuna mtu aliye timamu atakubali kushiriki uchaguzi kwa tume hii..

Serikali hii iache kujificha kwenye kivuli cha machafuko na fujo huku ikitakasa wizi inaoufanya kila baada ya miaka 5.
Your browser is not able to display this video.
 
ni muhimu sana wakashughulikiwa vizuri sana tena bila huruma Lakini bila kumunea mtu 🐒
 
Wajinga, watupe katiba mpya na tumehuru ya uchaguzi tuache kuandamana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…