Serikali yawapiga marufuku waganga (SIAJELEWA HAPA)

Serikali yawapiga marufuku waganga (SIAJELEWA HAPA)

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
Serikali yawapiga marufuku waganga

WAGANGA wa tiba za jadi nchini ,wanatakiwa kuacha mara moja kudanganya watu kuwa wanatibu magonjwa kama kifua kikuu, kisukari na Ukimwi kwa kuwa sheria haziwataki kujitangazana badala yake wanapaswa kutangazwa na wanaopata tiba na kupona.

Onyo hilo kali limekuja wakati maelefu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba kutoka kwa Mmchungaji mstaafu
Ambilikile Mwasapile.

Mchungaji huyo amekuwa akitibu magonjwa sugu yakiwemo kifua kikuu, kisukari, Ukimwi, degedege na shinikizo la damu.Onyo dhidi ya waganga, lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Lucy Nkya, katika hotuba yake kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kifua kikuu Duniani.

yaliyofanyika kitaifa mkoani Mara.
Alisema kuenea ugonjwa wa kifua kikuu unaenea kwa kasi kwa sababu wananchi wanakubali kudanganywa na waganga hao.

“Nasema kuanzia sasa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji, kuwadanganya wagonjwa kuwa wanatibu magonjwa kama hayo, maana mnadanganya watu na wanazidi kufa. Hatutaruhusu tena mchezo huo, narudia ni marufuku, tiba halisi inatolewa hospitalini si kwingineko," alisema Naibu Waziri.

Alisema waganga wazuri hawajitangazi na kwamba wanaopaswa kujitangaza ni wafanyabiashara tu ambao kazi yao kudanganya watu kwa kutumia matangazo mazuri mazuri.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo hakugusia tiba inayotolewa na Mchungaji Mwasapile, ambayo watu mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wamewahi kuitumkia.

Akizungumzia mikakati ya serikali kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu, alisema wizara imeanza kusambaza aina mpya ya darubini za kisasa za LED, zenye uwezo mkubwa zaidi wa kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi.

“Hadi kufikioa mwisho wa mwaka huu, asilimia 95 ya hospitali zote za wilaya, zitapata darubini hizi mpya na ifikapo mwishoni mwa 2012 hospitali zote zikiwemo za mashirika ya dini zitakuwa zimepata, vifaa vipya vya
kuoteshea vimelea vya kifua kikuu,”alisema na kuongeza.

Alisema vifaa hivyo vitafungwa katika maabara za Hospitali za Muhimbili, Mbeya, Bugando na Kibong’oto.

Alikiri kuwa wizara hiyo inakabiliwa na upungufu wa wataalam wakiwemo mafundi sanifu wa maabara na uelewa mdogo wa jamii kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu.

Source:
Mwananchi
 
Akiwemo babu wa Loliondo au hili katazo yeye halimhusu?
 
Alisema kuenea ugonjwa wa kifua kikuu unaenea kwa kasi kwa sababu wananchi wanakubali kudanganywa na waganga hao.

"Nasema kuanzia sasa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji, kuwadanganya wagonjwa kuwa wanatibu magonjwa kama hayo, maana mnadanganya watu na wanazidi kufa. Hatutaruhusu tena mchezo huo, narudia ni marufuku, tiba halisi inatolewa hospitalini si kwingineko," alisema Naibu Waziri.

Alisema waganga wazuri hawajitangazi na kwamba wanaopaswa kujitangaza ni wafanyabiashara tu ambao kazi yao kudanganya watu kwa kutumia matangazo mazuri mazuri.

Hivi huyo Waziri anayo akili timamu??? How dare can he/she utter such words. Eti wafanyabiashara wanaotoa matangazo yao wanadanganya! Hivi anazijua sheria za matangazo ya biashara?? Kwa hiyo coca cola, pepsi, voda, airtel, tigo, foma gold, etc wote wanadanganya? Ama kweli serikali ina watu bom bom hivi huwa hawajiandai??
 
Hii ni kweli wafanyabiashara wote ni waongo, they never spill all the truth its a mind game and they know how to play it well! Unadhani cocacol, voda, tigo, foma gold au hata hao wengine sio waongo?? Uzuri ni kwamba they know how to cover their track very well.... Kwa kuwa hapa sio mahala pake nadhani niishie hapo tuendelee kujadili haya ya waganga wa jadi (tiba za asili)
 
...Ila ni medical doctor?

Ndibalema, Babu wa Loliondo hayupo kwenye kundi la waganga wala kwenye medical Doctor, give him another name.
Vizuri ni kwamba katika watu wanaompinga wewe ni mmoja wao!! ila bado hujamjua vizuri. pole mkuu
 
Hivi huyo Waziri anayo akili timamu??? How dare can he/she utter such words. Eti wafanyabiashara wanaotoa matangazo yao wanadanganya! Hivi anazijua sheria za matangazo ya biashara?? Kwa hiyo coca cola, pepsi, voda, airtel, tigo, foma gold, etc wote wanadanganya? Ama kweli serikali ina watu bom bom hivi huwa hawajiandai??

matangazo ya biashara yanadanganya.acha ubishi wewe.
 
Wa Lolionda kapasishwa na vigogo wa ccm kwani kawatibu wengi ngoma!!:juggle:
....na si wa ccm tu! wengi wa wanasiasa wa nchi hii.. maana wengine wamekodi helkopta kupeleka watu!!! (kilichobadilika pale ni kule kuitwa Mchungaji mstaafu!) vinginevyo shehe yuleyule kanzu tu imebadilika!! (wanakataa waganga wa kienyeji huku wanawapokea kwa jina jingine!)

Yaani akili za kitanzania.... saa zingine sielewigi!
 
wa loliondo, pamoja na ndodi ni waganga wa kienyeji tu, si wa tiba mbadala? au? kwani si anatumia mzizi?
 
Back
Top Bottom