Pre GE2025 Serikali yazindua kamati ya ushauri wa Kisheria bila malipo, kutatua migogoro ya kisheria inayosababisha baadhi ya wananchi kuishitaki serikali

Pre GE2025 Serikali yazindua kamati ya ushauri wa Kisheria bila malipo, kutatua migogoro ya kisheria inayosababisha baadhi ya wananchi kuishitaki serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchini imezindua kamati maalumu ya ushauri wa kisheria na kliniki ya sheria bila malipo mkoani Mwanza ikiwa ni hatua ya serikali ya kutatua migogoro ya kisheria inayosababisha baadhi ya wananchi kuishtaki Serikali.

Akizungumza jijini Mwanza Mkaguzi wa huduma za uratibu na ushauri wa kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Neema Ringo amesema kwa mwaka ofisi hiyo imekuwa ikipokea zaidi ya kesi 500 kutoka kwa wananchi wanaotaka kuishtaki serikali. Hii ni kutokana na kutoridhishwa na huduma zinazotolewa na baadhi ya viongozi na watumishi wa serikali hivyo kwa kuliona hilo serikali imeamua kuja na kamati hiyo ili kushughulikia kesi hizo.

 
Back
Top Bottom