Librarian 105
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 261
- 356
Utangulizi:
Mahitaji ya walimu nchini hadi kufikia lengo la uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi 1:50 ngazi ya shule za msingi na 1:20 kwa ngazi ya shule za sekondari kulingana na Mpango wa III wa Maendeleo wa miaka mitano. Yanaweza kufanikiwa pasina kuathiri uchumi wa nchi endapo serikali itaamua kuanzisha programu itakayotengewa 3% ya bajeti kila mwaka na kisha kuajiri walimu ndani ya miaka mitano mtawalia. Ni maamuzi tu ya sera sahihi za kuamua uelekezaji wa rasilimali za nchi zenye kubeba mitazamo chanya ya kiuchumi yanakosekana. Huku hofu ya kuongeza matumizi ya kawaida ya serikali ikichukua nafasi zaidi hata kusababisha ukubwa wa tatizo kuzidi kuwa kubwa siku hadi siku.
Tatizo la upungufu wa walimu nchini kwa mujibu wa Ofisi ya rais, tamisemi mwaka 2023 unaonyesha ni zaidi ya nusu ya idadi ya walimu waliopo mashuleni. Kwa mantiki hiyo, ili kuiishi Tanzania Tuitakayo kwenye sekta ya elimu, upo ulazima wa kimuundo na kisera wa kutenga 3% ya bajeti za serikali kwa ajili kuajiri walimu. Mathalani, kwa rejea ya bajeti ya mwaka huu ingawa bado hajaidhinnishwa na bunge, makadirio ya bajeti nzima ya nchi ni takribani trilioni 49. Ukikokotoa ile 3% unapata wastani wa trilioni 1.47.
Hili ni fungu la fedha ambalo serikali ingeweza kujipanga nalo kuajiri walimu wengine wapya kwa kutenga mishahara yao ya mwaka mzima pamoja na stahiki zao zingine wanazopaswa kulipwa kama watumishi wengine wa umma. Utaratibu huu ukiwa, kwa mfano waalimu wapya wakawa waajiriwa 90,000 wa ngazi ya TGTS B1/TGTS C1 au TGTS D1 kwa kuanza na mshahara wa kima cha chini, ndani ya miaka mitano mtawalia sekta ya elimu ingeweza kuwa imepunguza walau 85% ya tatizo la upungufu wa walimu nchini. Kisha serikali itasimama kuajiri ili kuelekeza fungu hilo (3% ya bajeti ya kila mwaka) kwenye maeneo mengine ili kuzidi kuboreshea miundombinu yake ya kujifunzia na kufundishia kwa shabaha ya kuzidi kukuza kiwango na ubora wa elimu kwenye fani mbalimbali za kitaaluma na stadi za kimaisha.
Wakati fulani waziri alipata kusema hali ya uchumi wa nchi hairuhusu kuajiri walimu kuendana na mahitaji yaliyopo. lakini, kwa hakika, serikali ina mamlaka kamili ya kubana matumizi ikiwemo pia kupunguza ukubwa wa posho za watumishi wake,au kusitisha na kubadilisha matumizi ya mafungu ya miradi ya umma yasiyo na tija kitaifa ili kuokoa sekta ya elimu nchini. vile vile haishindwi kuiongezea fungu la asilimia hiyo Wizara ya Elimu au Wizara ya nchi Or-Tamisemi kufanikisha programu hii kwa ufanisi. Isitoshe pia ina vyanzo vya mapato ya ndani ambavyo vimekosa udhibiti wa kukusanywa kodi zake ambazo kwazo nazo zingetumika kuanzisha programu yenye kulenga kutatua kero za uhaba wa walimu. Kinachokosekana hapa, ni utashi wa vyombo vya maamuzi na wasimamizi wa sera za kifedha serikalini, kuwa sehemu ya tatizo linaloikabili sekta ya elimu.
Wanachangia kwa njia ya uelekezaji usiofaa wa rasilimali za taifa kwenye mikakati ya kupambana na ujinga nchini kwani kuna maeneo mengi ya umma fedha zinapotea kwa ufisadi na ubadhirifu lakini uwajibikaji upo chini mwaka hadi mwaka. Lau kwama fedha hizo zingetumika kuajiri walimu, moja kwa moja zingeingia kwenye mzunguko wa fedha wa nchi na pia kupunguza makali ya ukosefu wa ajira, na kwa upande wa kielimu kungepatikana matokeo chanya kwa kiwango kikubwa.
Maeneo mengine ambayo yanao mchango mkubwa wa kutatua kupunguza makali ya uhaba wa walimu ni; mipango ya muda mfupi ya maendeleo pia kuainisha kwa kina kiasi cha mafungu ya fedha yanayohitajika na vyanzo vya mapato yake kutengwa mapema kimkakati. kuboresha kampeni za uzazi wa mpango kwa kuasisi motisha za zawadi watakazotunukiwa kaya zenye kiwango fulani cha watoto kila mwaka ili kudhibiti kasi ya ongezeko la watu kutegemeana na uwezo wa serikali kutoa huduma za kijamii.
Hali kadhalika, itungwe sera ya ongezeko la watu yenye kutoa miongozo kwa serikali na raia wake katika mashirikiano yao ya kujenga taifa, kwenye kusimamia na kutekeleza mipango ya taifa ya muda mfupi na muda mrefu kutokana na kuja kujumuishwa kwake kwenye sensa ya taifa.
Hitimisho
Utaratibu wa kutenga 3% ya bajeti ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano kwa malengo ya kuajiri walimu wapya kila mwaka, ni aina ya mkakati wenye tija kitaifa kwa ustawi wa kijamii na kiuchumi, wenye kusisitiza katika usimamizi na uendeshaji wa programu zake kutegemea maamuzi sahihi ya serikali ya kutumia vyema mgawanyo wa pato ya taifa kimkakati. Kwa mnasaba wa kuboresha utoaji bora wa elimu nchini kwa shule za umma bila kutegemea misaada ya hisani na mikopo.

Upvote
0