Tetesi: Serikali za Kiafrika ndo sumu ya maendeleo ya chi za kiafrika

Tetesi: Serikali za Kiafrika ndo sumu ya maendeleo ya chi za kiafrika

Capital

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,468
Reaction score
1,063
Ndugu wanabodi

Mtakumbuka kuwa bara la Afrika lilikumbwa na jinamizi la utumwa na baadaye ukoloni na baadaye sana ukoloni mambosasa ambao bado tunaathirika nao na mwishowe haujulikani hadi sasa.

Miaka ya sitini, nchi nyingi za Afrika zilipata uhuru. Uhuru ambao ulishindwa kubadilisha chochote katika nyanja za kiuchumi, kisayansi na kielimu na kiafya. Miaka karibia sitini, watu wengi wa Afrika ni maskini zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Hawana elimi na kwa walio na elimu basi hiyo elimu si chochote na wala si lolote. Elimu iliyoshindwa kubadilisha hali za jamii za kiafrika kwa miongo sita sasa.

Kwa vipindi mbalimbali, waafrika wamekuwa wakiunda serikali zao ambazo kwa kiwango kikubwa, zimeshindwa kuyaishi matumaini na kuziishi ndoto za waafrika. Nitajikita katika mada yangu nikiiongelea Tanzania.

Tukiachana na historia, nchi yetu imekuwa inafanya vibaya kwa kila nyanja. Afya, elimu, michezo,;uzalishaji mashambani na viwandani.. yaani huko kote ni sufuri. Sasa hivi nchi ina watu wasiopungua milioni 50.. ambapo karibia nusu ya hao ni vijana. Vijana hawa hawajaandaliwa kielimu ili kuweza kupambana na changamoto za kimaisha. Serikali ipo, haina dira wala uelekeo kwa ajili ya hawa vijana. Watanzania kama walivyo raia wa nchi zingine, ni wabunifu sana kwa kadri kila mtu alivyojaaliwa, serikali ipo na haina mpango wa kutumia ubunifu wa ndani kutatua matatizo ya ndani. Serikali huku ikijua fika kuwa ni wajibu wake kuweka mazingira bora ili watu wote wachangie katika uchumi wa kitaifa, yenyewe iko bize na kauli za kilaghahi za upembuzi yakinifu, michakato.. nk nk. Serikali haitafuti pesa kwa ajili ya kuwekeza katika majukumu ya msingi kama vile kutoa elimu na afya bora, yenyewe ipo kufikiria uchaguzi unaofuata.. Bado watoto wa kitanzania wanakaa chini, tena chini ya miti kwa madai hiyo ndo elimu.

Ukitizama sekta nzima ya elimu hutashangaa yanayotokea hapa nchini. Waliopitia shule na vyuo mbalimbali wanaonekana hamna kitu.. yaani hawana tofauti na waso ma elimu. Nenda halmashauri, mawizarani.. utaona ninachokisema. Watu wasoelimika ndo wanaofanya maamuzi.. bilashaka matokeo ya mauzi hayawezi kuwa na maana..

Afya.. watu wasoelimika vyema aghalab watatenda vyema katika maamuzi. Serikali kila mwaka inasingizia haina pesa.. huku kila baada ya miaka mitatu au mitano utaskia kashfa za ajabu za wizi qa pesa za serikali.. na wanaoiba hawafanwyi chochote. Matokeo ni kwamba watu wengi hupata madhara kiafya kutokana na matatizo madogo madogo ambayo yangetatuliwa kirahisi kabisa.. mambo kama fistula.. ulemavu kwa watoto na vitu kama hivyo.

Serikali kutojiamini ni tishio kwa ustawi wa nchi. Serikali inapokuwa haijatenda ipasavyo na inahisi watu hawaridhiki na utendaji huanza kujihami kwa luwanyanyasa wananchi.. mfano rais kwa hofu yake binafsi anaamuwa kuwanyanyasa wapinzani wake hata kama hakuna sababu.

Mwishowe, watu wa Afrika wanaonekana ni ziro kabisa. Vijana wanaamua kuvuka bahari kuu kwa mtumbwi pamoja na hatari kibao zilizoko mbele. Vijana wanaoenda kufagia bara bara kimsingi wanakimbia hali mbaya nchini mwao.. hata kama wanajua hatari iliyopo mbele kwa kufanya hivyo.

Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi zilipitia katika changamoto nyingi hata kusababisha mauaji ya kimbari. Lakini nchi nyingi zilitumia muda mfupi kurudia hali ya kawaida na kukua na kuwa super powers. Mifano iko mingi. Lakini nchi za kiafrika mtu anazaliwa na anafariki bila kupata nafuu ya maisha. Kwa mfano, waliozaliwa mwaka 1961 Tanganyika sasa wana miaka 56.. hali ya maisha ni ile ile.. ya hovyo hovyo.

Je kwa nini tusiamini kuwa viongozi wa kiafrika na Tanzania ni majipu, wasiojuwa jinsi ya kututoa tulipokwamia? Na kwa nini tusiamini kuwa hawa viongozi ni geresha tu hawana mbinu wala ufundi wa kuifanya Afrika kutoka kuchekwa na kuwa ya kupigiwa mfano?

Naomba kutoa hoja
 
Back
Top Bottom