Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna wakati, mambo mabaya hutokea yakiwa yamebeba dhamira njema. Watu wa imani wanalifahamu hili. Yawezekana ukawa unataka kusafiri kwa basi, usiku ukaugua ghafla, ukasikitika sana kwa sababu hutaweza kusafiri. Lakini basi hilo hilo ulilotaka kusafiri nalo likapata ajali. Wewe ukawa umesalimika kwa sababu ya kutosafiri nalo, jambo lililosababishwa na kuugua kwako, ulikokuona ni bahati mbaya sana.
Fikiria CCM ingetenda haki kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, watu wote wangeamini kuwa CCM chini ya Samia imebadilika, na inawezekana kabisa watanzania wangepumbazika na uchaguzi wa mwaka huu, wakiamini kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Lakini kwa bahati nzuri, nina imani Mungu aliitia upofu CCM, ikafanya uharamia, udhalimu, uchafu mpaka mauaji ya raia ili kuupora uchaguzi wa Serikali za mitaa. Hali ile imeamsha hamasa, na kupeleka ujumbe kwa raia kuwa kumbe CCM na Serikali, chini ya Rais Samia, katika demokrasia, haki na usalama wa raia ni mbaya kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo katika nchi hii. Yaani mpaka kufikia kuua watu kwaajili ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kitongoji. Hali hii imewafanya wananchi kuielewa CCM na Samia katika uhalisia wao. Kwa sasa hakuna mwenye imani tena kuwa kunaweza kuwa na uchaguzi huru na wa haki chini ya uongozi wa Samia. Hii imezidisha hasira dhidi yake na dhidi ya CCM.
Baada ya kupewa ujumbe wa wazi kupitia uchaguzi wa Serikali za mitaa, tukatae kuchezewa utu na ubinadamu wetu.
NO REFORM NO ELECTION
BILA YA MABADILIKO HAKUNA UCHAGUZI.