Serikali za mtaa Buguruni Sheli

gileun

Member
Joined
Nov 8, 2017
Posts
85
Reaction score
74
Mambo vipi guys. Naomba kujua zilipo ofisi za serikali ya mtaa pale Buguruni sheli. Kwa anaejua tafadhali nijulishe nahitaji kufika lakini sifahamu zilipo!
 
Unatokea sehemu gani?fika buguruni chama pale pale angalia jengo lile la mama lishe pale pale pemben utaona bango la ofisi ya serikali ya mtaa!!!
 
Mambo vipi guys. Naomba kujua zilipo ofisi za serikali ya mtaa pale Buguruni sheli. Kwa anaejua tafadhali nijulishe nahitaji kufika lakini sifahamu zilipo!
Upo sehemu gani muda huu ?
Nipo Karume nataka nikupitie na hii VX nikupeleke ilipo fidi hadi mlangoni mkuu
 
Mambo vipi guys. Naomba kujua zilipo ofisi za serikali ya mtaa pale Buguruni sheli. Kwa anaejua tafadhali nijulishe nahitaji kufika lakini sifahamu zilipo!
Kwanza naona kama unachanganya sehemu mbili tofauti.. Hapo Buguruni shells kuna ofisi ya mtendaji kata ya Buguruni. Ukisimama hapo shells ukitazama upande wa pili wa barabara utaiona.

Lakini kama unataka kwenda ofisi ya serikali ya mtaa, kwa kutokea hapo shells ina maana unataka kwenda ofisi ya mtaa wa Buguruni Kisiwani. Ni karibu pia na hapo shells. Ulizia sehemu inaitwa Y2K au stendi ya magari ya mbezi na muhimbili. Ukifika hapo utaliona bango limeandikwa Ofisi ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Buguruni.

Kutoka hapo shells mpaka hapo ofisini ni mwendo wa dakika 3 tu.
 
Ahsante sana kaka, maelezo haya ni msaada sana! Ubarikiwe
 
Mkuu ndo hapo umepatia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…