Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar zatoa azimio

Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar zatoa azimio

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
[h=3][/h]


Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar zatoa azimio la kuwataka wanafunzi na vijana kuweka mbele maslahi ya nchi kwa kuelimishana na kuhamasishana juu ya haja ya kuirudisha Jamhuri ya Watu Wazanzibar na Muungano wa mkataba ili Zanzibar iwe na mamlaka kamili.


Azimio hilo lilitolewa kwenye kongamano lililofanyika juzi Jumamosi katika ukumbi a Salama Hall Bwawani. Zaidi ya wanafunzi mia tano na ishirini walihudhuria kongamano hilo pamoja na kuwa lilifanyika katika kipindi cha matayarisho ya mwisho ya eid.


Hii ni kuonesha ni kiasi gani wanafunzi wa vyuo na vijana wameamka katika harakati za kuitetea nchi yao na kutaka Zanzibar iliyo na mamlaka kamili na muungano wa mkataba.



Watoa mada katika kongamano hilo alikuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ndugu Ibrahim Mzee, Mhadhiri kutoka SUZA ndugu Ali Vuai, Mtaalam wa mambo ya Uchumi ndugu Mselem Khamis Mselem. Pia Bi Naila Jidawi nae alieleza machache.


Nae Mwakilishi wa Kiembesamaki Mh. Mansor Yussuf Himid alipoingia kwenye ukumbi huyo kama mualikwa alishangiriwa na wanafunzi na vijana kwa makofi na hoihoi na kuombwa azungumze japo machache na wanafunzi hao walionekana kuwa na hamu ya kumsikia Mwakilishi huyo waliozoea kumuona akinguruma barazani kupitia vyombo vya habari.


Pamoja na michango mingi ya wanafunzi na vijana hao, nao walimpongeza Mwakilishi Mansour pamoja na Wawailishi wengine walioonesha moyo na ujasiri kama wake wa kuitetea Zanzibar na kuahidi kuwa wataendelea kuwaunga mkono na wako pamoja nao bega kwa bega.


Walisema kuwa zama za kutishana zimepitwa na wakati. Huu ni wakati wa hoja hasa wakizingatia wao ni vijana wasomi wa Zanzibar.


Azimio pia liliitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba izingatie misingi ya kuyaheshimu maoni ya wananchi juu ya aina gani ya muungano wautakao.


Azimio hilo pia lililaani vikali vitisho vinavyotolewa na baadhi ya wanasiasa wachache wenye kulinda maslahi yao binafsi badala ya yale ya waanchi na taifa kwa ujumla.


Katika wageni waalikwa maamiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiiskam nao walihudhuria ambapo waliwakilishwa na Amir Mselem


Imewekwa na MAPARA at 11:31 PM
 
Kumbe wanafunzi wa zanzibari!
Basi ya wazanzibari yaamuliwe kizanzibari!
 
Muungano wa mkataba wa nini? Sisi hatuwataki waz'bar, daini tu nchi yenu mtuache na Tanganyika yetu.
 
Awareness ni muhimu sana kwa maendeleo ya kikundi fulani.
 
ni vzr kama wanaungana kutetea maslahi ya nchi yao.
Vijana wasomi ni nguzo muhimu ktk maendeleo.
Wawe makini tu wasije wakatumika vibaya.
 
hongereni kama kweli mliyo yaongea mtayatekeleza na kuwa na moyo wa uzalendo
 
Back
Top Bottom