Serikali Zanzibar kuendelea kuwahudumia majeruhi ajali iliyoua wanne Shinyanga

Serikali Zanzibar kuendelea kuwahudumia majeruhi ajali iliyoua wanne Shinyanga

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Unguja. Makamu wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali itaendelea kuwahudumia majeruhi waliopata ajali katika basi la kampuni ya Classic mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo ilitokea Juni 2, 2021 katika kijiji cha Buyubi kata ya Didia mkoani Shinyanga baada ya dereva wa basi hilo lililokuwa likitokea nchini Uganda kupinduka na kusababisha vifo vinne na wengine 20 kujeruhiwa.

Katika ajali hiyo wengi walikuwa ni wanafunzi kada ya afya wakitokea Chuo Kikuu cha Bugema kilichopo Kampala nchini Uganda.

Akizungumza baada ya kuwatembelea majeruhi watano waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo Jumatano Juni 23, 2021, Abdulla amesema Serikali zote mbili zitaendelea kushirikiana kwa karibu kuhakikisha afya za majeruhi hao ambao ni watumishi wa Serikali ya Zanzibar zinaimarika.

“Niwaombe madaktari waendelee kuwahudumia, na serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia mratibu wake anayesimamia shughuli za serilikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la wawakilishi aliopo Dar es salam ataendelea kutoa ushirikiano unaohitajika,” amesema

Pia, amewataka madaktari wanaowatibu majeruhi kutofanya haraka kuwaruhusu mpaka watakapojiridhisha kuwa afya zao zimeimarika.

Naye daktari bingwa wa mifupa wa hospitali hiyo, Victoria Munthali amemuahidi kiongozi huyo kuwa wataendelea kuwahudumia mpaka afya zao zitakapotengamaa.
 
Hao ni wa SMZ wetu hata maiti haitoki pale kwa mazishi hata kama imebakia 5/- ya kinachosemekana ni deni.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom