#COVID19 Serikali zinazojali wananchi tutazijua kupitia Corona

#COVID19 Serikali zinazojali wananchi tutazijua kupitia Corona

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Kuna nchi 2 East Africa zinaamini corona ni mapepo na wenye dhambi ndio wanapata.

Hakuna hatua zinachuliwa nchi 3 makini east africa zimefunga mipaka, zimezuia raia kusafiri, zimezuia public transport, lakini nchi ya wachapakazi africa nzima inasema hakuna corona.

Serikali inayo jali wananchi wake huu ndio wakati wa kuonyesha kinga ni bora kuliko tiba.

Hadi sasa wanachi hawajui wamsikilize nani, kila mmoja anaongea anacho jua, bashite naye ameona ni sehemu ya kutokea.

Ivi hawa viongozi hawajui kwamba hata wao likiwakuta hakuna kwenda India wala ujeremani?

20200325_211815.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walitakiwa wafanye maamuzi.mapema..

1.funga mipaka
2. Funga shule vyuo
3. Wafanyakazi wote work from home
4. Tnasport : zuia..
5. Testing centers every district
6. Masks and temprature test kits availability.
Maamuzi magumu Bongo ni katika kushughulikia wapinzania tu na sio kwenye issue sensitive kama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walitakiwa wafanye maamuzi.mapema..

1.funga mipaka
2. Funga shule vyuo
3. Wafanyakazi wote work from home
4. Tnasport : zuia..
5. Testing centers every district
6. Masks and temprature test kits availability.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila mtu ni mtaalamu sasa
Haya anza wewe kujifungia nyumbani kwako
Na biashara yako hiyo ya kutembeza vyombo sijui uta survive kwa wiki ngapi
 
Nawashangaa hadi leo mnaokomaa work from home... Hebu tupe mfano wa kazi tz unazoweza kuwork from home
 
Kwanini tusichukue hatua wenyewe?! Yaani kwa kuona hatari tuliyonayo, wewe amua kuji-lockdown.
 
Gharama za maisha zinaenda kuongezeka sana.

US wametoa $ 2 T.. Kuhakikisha wanalinda mifuko ya watu.
 
Kuna nchi 2 East Africa zinaamini corona ni mapepo na wenye dhambi ndio wanapata.

Hakuna hatua zinachuliwa nchi 3 makini east africa zimefunga mipaka, zimezuia raia kusafiri, zimezuia public transport, lakini nchi ya wachapakazi africa nzima inasema hakuna corona.

Serikali inayo jali wananchi wake huu ndio wakati wa kuonyesha kinga ni bora kuliko tiba.

Hadi sasa wanachi hawajui wamsikilize nani, kila mmoja anaongea anacho jua, bashite naye ameona ni sehemu ya kutokea.

Ivi hawa viongozi hawajui kwamba hata wao likiwakuta hakuna kwenda India wala ujeremani?

View attachment 1399351

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukijifungia wewe ukaishi milele inatosha acha sisi tuchape kazi kwa sababu tunaamini kufa ni mara moja tu

Sent using IPhone X
 
Hiyo blogging na youtubing unaifanya bila kwenda nje kupiga picha na video?

Ndiyo, mbona habari mitandaoni zipo nyingi sana!!! Unaweza ukatengeneza makala za viongozi, habari za wasanii mitandaoni, breaking news za duniani, aisee kuna mambo mengi sana online yanaweza kufanikishwa bila hata kutoka nje na camera.
 
Sasa hapo habari moja mnaitoa watu wangapi...wewe ushajaribu kufanya kwa njia hiyo ukafikia hatua ya kulipwa na YouTube? Mambo si mepesi hivyo ndugu... Watu wanachaneli za YouTube na blogs wanatafuta sana camera... Ukianza kuchukua picha zilizopigwa na wengine na kuiba contents zao utajikuta matatani bure.
Ni kheri ungesema freelancing na ambayo hata hivyo wabongo tumelala mno.
 
Back
Top Bottom