Serious Water Project Funders

Serious Water Project Funders

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,662
Habari zenu wadau,

Tumeanzisha project ya maji kwa lengo la kuwapatia wananchi wa vijijini maji safi na salama (wananchi wameisubiri serikali tangu uhuru bila mafanikio, tukaona ni busara tuwanusuru). Tumeweza kukodisha machine na kuchimba maji 80 m deep, yakatoka mengi ajabu (angalia picha), pamoja na kutengeneza miundo mbinu mingine kwa gharama ya Tshs 25,000,000 mpaka sasa. Pia tutanunua water pump kwa hela zetu wenyewe.

Tumenunua eneo kuzunguka kisima, eka kadhaa kwa ajili ya kukuza miti, mboga, nk., hii itatoa ajira kwa watu mbalimbali licha ya kuboresha mazingira na afya za watu. Baada ya kufanya tathmini ya awali tumegundua kuwa maji ni mengi sana, kwa hiyo tunataka tuyasambaze kijiji kizima. Kwa nguvu zetu peke yetu ni kazi kubwa sana, kwa maana hiyo naomba anayefahamu taasisi ambayo iko "serious" na inatoa hela kwa ajili ya miradi ya maji nchini Tanzania ili tuweze kushirikiana nayo. Tumeanza na kijiji chetu.
 
Attachments

  • Water_1.jpg
    Water_1.jpg
    379.7 KB · Views: 351
  • Water_2.jpg
    Water_2.jpg
    329.2 KB · Views: 322
  • Water_3.jpg
    Water_3.jpg
    403.7 KB · Views: 265
NB: Wadau wanaofund water projects hatutawaomba hela kama njugu, tutawaandikia proposal.
 
Kijiji gani?!je maji mnagawa bure au kuna contribution au yanalipiwa na users.Nakushauri hiyo proposal peleka mwenyew kwenye organization kama EU au wabelgiji na baadhi ya embassy kama za EU countries. Wakiona potential wanaweza kufund
 
Kijiji kipo Singida vijijini. Maji yatalipiwa kidogo, vinginevyo itakuwa ngumu kuendesha mradi, kumbuka gharama zote mpaka sasa ni za kwetu.
 
Andaa proposal yako vizuri lakini nakushauri usiweke gharama kubwa ya uchangiaji wa maji maana Funders wanaweza kukukatalia.

Jaribu kumpelekea Muhindi flani ivi anaitwa Sudat kama sikosei alikuwa na project ya kuchimba visima mikoani....,Ikishindikana wafate wanasiasa wakubwa hasa wa CCM kama Edward Lowasa naamini watakupa maana naona wanajiandaa kwa uchaguzi so ili kuchochea wapate kura lazima wataku- fund

Ni ushauri tu Mkuu.
 
Hahahaaa, EL! Hebu naomba details za huyo Muhindi kama ukizipata vema, hata kwa PM. Ahsante kwa ushauri mkuu.
 
Usithubutu kufanya project serious na wanasiasa. You will be kicked out na wao kujifanya ndio waanzilishi ili hali waweze kushinda chaguzi mbalimbali. Hata wahindi kuwa nao makini vilevile; nakushauri watafute hawa jamaa wanaojiita WaterAid. Hii ni NGO ina operate nchi nyingi kusaidia miradi ya maji. Makao makuu ni uingereza.
Andaa proposal yako vizuri lakini nakushauri usiweke gharama kubwa ya uchangiaji wa maji maana Funders wanaweza kukukatalia.

Jaribu kumpelekea Muhindi flani ivi anaitwa Sudat kama sikosei alikuwa na project ya kuchimba visima mikoani....,Ikishindikana wafate wanasiasa wakubwa hasa wa CCM kama Edward Lowasa naamini watakupa maana naona wanajiandaa kwa uchaguzi so ili kuchochea wapate kura lazima wataku- fund

Ni ushauri tu Mkuu.
 
Hiyo mitambo ya kuchimbia umeipata wapi na inagharimu bei gani kwa kisima?
 
Kama upo serious tuingie partnership

Nina sponsor wa hizi project kwa tanzania nina org mbili na international nina organ tatu

Nilikuwa na project kama hii lakini niliishia katikati baada ya kupata usumbufu wa serikali katika kufanya registration

Ila project yangu ilikuwa free of charge kwa wanakijiji watakao tumia hayo maji

Kama huko interested in partnership niPM otherwise unaweza kuendelea na project yako
 
Hiyo mitambo ya kuchimbia umeipata wapi na inagharimu bei gani kwa kisima?

Hiyo mitambo inapatikana Arusha, gharama ya kuchimba inategemea na sehemu unayotaka kuchimba na Hydrogeological and Geophysical report - survey.
 
Water Aid Tanzania,wacheki tena walikua wanataka watu wa maeneo ya huko waombe pesa kwa Mradi wa WASH,binafs nilikosa kwa uzembe wangu,wapo Msasani Peninsula Mkabala na Namibia Embassy,hongera sana kwa initiatives zako
 
Watafute pia JUST A DROP, MIMI NILISHAWAHI KUWAANDIKIA PROPOSAL KWA AJILI YA VISIMA HUKO KYELA (KIJIJI FULANI), WENYE KUTEKELEZA MRADI (HALMASHAURI) WAKASHINDWA KUSUBMITT MAPEMA REQUEST FORM ILIYOTAKIWA KUJAZWA NA DISTRICT WATER ENGINEER.
 
Kijiji kipo Singida vijijini. Maji yatalipiwa kidogo, vinginevyo itakuwa ngumu kuendesha mradi, kumbuka gharama zote mpaka sasa ni za kwetu.

Hongera zenu wakuu namimi natafuta fursa hapo...naomba utaratibu niwaSUPPLY mabomba na Vifaa vyake niko DAR,,,,!!
 
Andaa proposal yako vizuri lakini nakushauri usiweke gharama kubwa ya uchangiaji wa maji maana Funders wanaweza kukukatalia.

Jaribu kumpelekea Muhindi flani ivi anaitwa Sudat kama sikosei alikuwa na project ya kuchimba visima mikoani....,Ikishindikana wafate wanasiasa wakubwa hasa wa CCM kama Edward Lowasa naamini watakupa maana naona wanajiandaa kwa uchaguzi so ili kuchochea wapate kura lazima wataku- fund

Ni ushauri tu Mkuu.

mkuu ni lowasa yupi unasema, kuna watu wanaomsifu sana lowasa lkn nilipotembelea monduli vijijin mswakin juu na chini nilistaajabu. Hakuna hata tone la maji na yakipatkan ni ya kufwata na punda 8-10hrs na machafu yasiofaa kwa binadam. Cha ajabu bado wako wanaoona hilo si tatizo
Tushukuru wafadhili wa kanisa wanaohangaika kuvipatia hivo vijiji maji si lowasa alieshindwa kuwachimbia hata cha maji ya mifugo yao
 
Daa mkuu mi naonaga anamwaga mihela kwenye vikundi mbalimbali kuwasaidia wajasiriamali wadogowaodogo,wakina mama,makanisani na miskitini nikafkiri kwao kamaliza kumbe bado majanga.Kweli siasa mchezo mchafu!:lying::lying:
 
Ndivyo siasa ilivyo; Umahiri wa mwanasiasa ni pale anapoeza kusoma alama za nyakati jinsi watu wake wanavoeza kum challenge na yy hutumia ujanja wowote kujarbu kasolve hizo chalenge. Kama hapati challenge hakika hatafanya chochote. Akiona mnamshangia hata kama kajinyea amezungukwa na nzi hakika anajua hamuitaji kufanyiwa chochote na maisha yanaendelea kwingine kunako challenge
 
Mtafute tu MR. MUSTAFA SABODO; Email address: sabodo786lindi@yahoo.com
Ofisi yake ipo pale kwenye mzunguko wa Clock Tower nyuma ya Taxi zinazopaki pale na Ipo ndani ya lile jengo linalouza vifaa vya elekroniks vya jumla vya HISENSE 1969.
 
Hongera zenu wakuu namimi natafuta fursa hapo...naomba utaratibu niwaSUPPLY mabomba na Vifaa vyake niko DAR,,,,!!

Mkuu mabomba, PVC pipes diameter inchi 2 na inchi 2.5 unauzaje kwa mita? Unaweza kunipm.
 
Back
Top Bottom