Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,662
Habari zenu wadau,
Tumeanzisha project ya maji kwa lengo la kuwapatia wananchi wa vijijini maji safi na salama (wananchi wameisubiri serikali tangu uhuru bila mafanikio, tukaona ni busara tuwanusuru). Tumeweza kukodisha machine na kuchimba maji 80 m deep, yakatoka mengi ajabu (angalia picha), pamoja na kutengeneza miundo mbinu mingine kwa gharama ya Tshs 25,000,000 mpaka sasa. Pia tutanunua water pump kwa hela zetu wenyewe.
Tumenunua eneo kuzunguka kisima, eka kadhaa kwa ajili ya kukuza miti, mboga, nk., hii itatoa ajira kwa watu mbalimbali licha ya kuboresha mazingira na afya za watu. Baada ya kufanya tathmini ya awali tumegundua kuwa maji ni mengi sana, kwa hiyo tunataka tuyasambaze kijiji kizima. Kwa nguvu zetu peke yetu ni kazi kubwa sana, kwa maana hiyo naomba anayefahamu taasisi ambayo iko "serious" na inatoa hela kwa ajili ya miradi ya maji nchini Tanzania ili tuweze kushirikiana nayo. Tumeanza na kijiji chetu.