Service Center ya magari ya NISSAN

Service Center ya magari ya NISSAN

RJ-White

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2014
Posts
744
Reaction score
752
Habari wanaJF,
Nimenunua gari aina ya Nissan Terrano, naomba kujua kwa mtu anayefahamu garage au service center yenye mafundi wazuri kwa magari ya Nissan. Mafundi wengi wako vizuri kwa Toyota, ila nasikia Nissan sio kivile sana hasa kutokana na muundo na aina ya spare zake zilivyo. Ukiacha CFAO ambao naona ni ghali sana, kwa garage za kawaida ni ipi nzuri kwa hapa Dar es Salaam?
 
Mkuu mbona umenunua terrano au ni second hand. Terrano spare zake za kawaida ila zinasumbua mjini ni bora ungeamia Toyota, ila akija mshamba mpige nayo uchukue Toyota, alafu hiyo NT ni new model au za kizamani. Kama hela yako ya ualimu ni bora utafute mafundi wakawaida kama hela yako kama ya Bakhresa basi nenda pale kinondoni muslim karibu na soko la tx karibu na kanisa LA RC, pale full diagnosis and Wheel alignment.
 
Ualimu unahusiana nini na pesa yake? Acha ujinga wa ku lebel watu. Hata ungesema ya udaktar bado nsingeona uhusiano. Usiwe mpuuzi kwa kias kikubwa sana.
 
Habari wanaJF,
Nimenunua gari aina ya Nissan Terrano, naomba kujua kwa mtu anayefahamu garage au service center yenye mafundi wazuri kwa magari ya Nissan. Mafundi wengi wako vizuri kwa Toyota, ila nasikia Nissan sio kivile sana hasa kutokana na muundo na aina ya spare zake zilivyo. Ukiacha CFAO ambao naona ni ghali sana, kwa garage za kawaida ni ipi nzuri kwa hapa Dar es Salaam?
Nina uzoefu na Nissan Terrano, ni gari nzuri saaana hasa ktk stability yaani inatulia barabarani ni balaa unaweza kata kona na spidi 160+ na bado usifeel, unaweza tembelea 180 usisikie wala kuhisi upo ktk spidi hiyo inashawishi kukimbia muda wote. Pia ni gari imara sana ilipata mzinga lakini ingini wala haijaguswa. Niliwahi kugongwa nyuma haikuumia hata kdg japo aliyenigonga aliumia.Nilikuwa nayo ya kwanza nikauza nikanunua ya pili nayo nimeuza hivi karibuni na nina mpango wa kununua ya tatu. Hayo ni baadhi ya mazuri ya terrano, ubaya wake ni spea zina bei juu kdg ya toyota japo si ghali sana. Mm nilikuwa napeleka kwa fundi mmoja pale gerezani anaitwa frank ila ni muda kdg. Uzuri wake ukufunga leo hadi kuharibika tena inaweza kaa miaka. Kwa kifupi ni gari nzuri sana kwa mm ambaye nimeitumia huwezi linganisha na surf hata kdg.
 
Back
Top Bottom