muuza ubuyu
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 3,539
- 3,551
Hi JF,
Na imani mmepumzika majumbani kwenu baada ya kutoka church (wakristu) mkimalizia weekend yenu. Kutokana na uzoefu na elimu nzuri itolewayo bure hapa JF na wanaJF waungwana, ningependa kujuzwa yafuatayo;
Kwa kawaida sisi watu wa uchumi wa kawaida huwa tunanunua magari yaliyotumika (mtumba) haswa haswa kutoka japan. Magari haya huwa hatujui mtumiaji alikuwa analitumiaje na hata namna alivyokuwa analifanyia service/alivyo replace vile vitu muhimu. Sasa basi, kutokana na mazingira haya ningependa kujua ni vitu gani vya kuangalia ama kubadili kabisa (hasa gari likiwa above 100,000km) kabla ya kuanza kulitumia!
Katika pita pita zangu humu JF na uzoefu wangu mdogo wa kutumia gari, nimeona ni muhimu kufanya yafuatayo;-
Lakini pia inasaidia mtu kuchukua hatua za mapema ili aangalie gari lake asilitumie bila service ya maana na hivyo kuliharibu kabisa na hivyo kupoteza pesa alizo save miaka nenda miaka rudi ama kukopa ili aweze kujiokoa katika suala zima la usafiri!
Pia ningependa kujua na gereji gani nzuri na yenye uaminifu kwa hapa mwanza bila kujari gharama zao!!!
Nawasilia 'ubuyu' wangu!

- Kumwaga oil engine yote na kusafisha kabisa kwani magari mengine oil yake inakuwa imetumika mda mrefu bila kubadirishwa na hivyo kugandiana huko chini na kuzuia oil kupanda pindi engine inapowashwa.
- Oxygen sensor, wataalam wanashauri vitu hivi kubadirishwa ili kusaidia gari lako kutumia mafuta vizuri.
- Kubadirisha timing chain na kuangalia belts zote kama bado zipo kwenye ubora. Timing chain ndiyo sababu yangu mimi kuanzisha uzi huu kwani nimeona uzi humu JF unaoongelea kitu hiki kwani kuna mtu amepoteza jamaa yake kwa sababu ya timing chain kukatika na hivyo vitu vyote kugoma kufanya kazi. Na hili ni tatizo kubwa hasa likitokea kwenye magari yetu haya ambayo ni automatic.
- Vingine ni kama kucheki break system, steering, ubora wamatairi (usitishwe na upya wa matairi hujui yalikaa store kwa muda gani tangu kutengenezwa kwake, unaweza kuta tayari yalisha expire!)