Set pieces: Tatizo kwa Simba sc

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za mwaka mpya wakuu,
poleni na majukumu ya kujenga taifa letu nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

SET PIECES TATIZO KWA SIMBA : kwenye mchezo wa mpira inafahamika kama mipira ya kutenga.

Msimu wa 2016/2017 liverpool ilikuwa na tatizo kama hili 70% ya magoli waliyofungwa yalikuwa ya set pieces mpaka pale walipotafuta solution na kumsajili van dijk ndio tatizo likaanza kupungua na kuisha kabisa mpaka leo imebaki historia.

Kwa muda mrefu simba sc imeshindwa kulifanyia kazi tatizo hili la mda mrefu kuanzia mechi za CAF ,za league kuu mpaka juzi kwenye kombe la mapinduzi cup, simba wameshindwa kutumia nafasi hizo zinazotokana na mipira ya kutenga zikiwa upande wao na kuadhibiwa ikiwa kwa mpinzani.

Kama simba wasipo lifanyia kazi tatizo la set pieces basi hata kwenye kombe la shirikisho wapinzani wao watatumia udhaifu wao kwenye eneo hilo.
mechi zote ambazo simba amepokeo kipigo kwenye kombe la CAF goli zinatokana na mipira ya kutenga na cross kuanzia mechi ya al ahli ,as vita,na kaizer chief aina ya goli zinafanana hili tatizo lisipo fanyiwa kazi basi simba itaenda kuadhibiwa kwa makosa kama hayo.

NB: Wale wazee wanategeana kuruka angani.
 
Wenyewe wako bize na mapokezi ya Chama! Wanaamini huyo ndio mkombozi wao!
 
Kwa sentensi yako hiyo mi sijakuelewa vizuri kama unashauri simba wazitumie vizuri set pieces au wajue namna ya kuzuia ili tusifingwe? Any way!! Tuache kama ilivyo.. lakini ninachotaka kukuambia mwana utoh ni kwamba..simba wameset diffence yao kwa waledi mno kiasi kwamba huwezi kufananisha na timu yoyote ya ligi ya NBC haha east Africa.. simba iko taff Sana kwenye difence kuliko hata forward yake..mi nakushauri labda uwaonee huruma utoh ambao hawajui kama wana beki mbovu ambazo haziwezi kupambania kimataifa zaidi ya ligi ya ndani.. kama unabisha muda ni shahidi.. acha twende wote kimataifa ndo tutachuja mbivu na mbichi
 
Defence imara gani? Ilipokea kichapo kutoka kwa Mayele, kisha makhirikhiri wakawapasua, kisha ikapigwa na geita gold refa akawaokoa, na ilishawah kupasuliwa na Kaizer Chiefs 4-yai.

Hapo bado zile hamsa kutoka Al Ahly, etc
 
Defence imara gani? Ilipokea kichapo kutoka kwa Mayele, kisha makhirikhiri wakawapasua, kisha ikapigwa na geita gold refa akawaokoa, na ilishawah kupasuliwa na Kaizer Chiefs 4-yai.

Hapo bado zile hamsa kutoka Al Ahly, etc
Yaani wewe kweli huangalii historia, wale mabeki simba ilipofungwa ndo hawa? Wale wa Kaizer Chiefs ndo hawa? Simba beki yake imeimarishwa sana na ndo maana kuna mabadiliko makubwa sana upande wa beki Simba haifungwi hivi karibuni, kufungwa hakuepukiki hata kama kuna mechi 100 kufungwa utafungwa tu japo kwa mechi chache
 
Defence imara gani? Ilipokea kichapo kutoka kwa Mayele, kisha makhirikhiri wakawapasua, kisha ikapigwa na geita gold refa akawaokoa, na ilishawah kupasuliwa na Kaizer Chiefs 4-yai.

Hapo bado zile hamsa kutoka Al Ahly, etc
Kati ya beki ya Simba na ile ya Yanga ipi imeruhusu lango lao kufungwa goli nyingi hadi sasa?
Hata ukija kwenye mapinduzi cup Yanga kapigwa goli 2 katika mechi 2 Simba kafungwa 0 katika idadi hiyohiyo ya mechi
Hiyo inakufundisha nini?
 
Mimi nakubali 100% kwamba kwenye set pieces Simba ni timu isiyo kwenye level iliyopaswa kuwa whether ni kuzitumia kumwadhibu mpinzani au kudhibiti wapinzani wasifunge.Hii ni ishara kuwa kuna uzembe sana kwenye mazoezi ya Simba , huenda nguvu nyingi haijawekwa kwenye utaalamu wa set pieces ikiwamo na penati ndiyo maana timu inaonekana mbovu mno katika kitu hicho.
 
Yanga ndio wana defence nzuri sana.
Ndio maana kila msimu wanachukua Ubingwa wa Ligi ya NBC na kushiriki mashindano ya Kimataifa bila kufungwa na timu yoyote.
Nawapongeza sana kwakweli.
 
Simba kwenye faulo zote kuanzia Penati hawako vizuri.
Sijui hata kwenye mazoezi wanafanya kitu gani.

Na hawataki kujifunza kwa mwenzao NTIBAYONKIZA wa Yanga fc.
 
Kati ya beki ya Simba na ile ya Yanga ipi imeruhusu lango lao kufungwa goli nyingi hadi sasa?
Hata ukija kwenye mapinduzi cup Yanga kapigwa goli 2 katika mechi 2 Simba kafungwa 0 katika idadi hiyohiyo ya mechi
Hiyo inakufundisha nini?
Kwani katika andiko langu kuna sehem nimesema kua yanga ana defense nzuri kuliko simba?
 
Tatizo lipo kwenye CAF sio league goli zote simba amefungwa kwa set pieces.
 
Kweli mkuu watu wanaongelea ushabiki ila ukweli ndo huo hata mechi ya Galaxy juzi hapa goli zote ni set pieces ila wanachukulia kiushabiki sio kiuhalisia mapinduzi na league sio kipimo sahihi cha kusema tatizo limeisha.
 
Bado utaendea na hoja zako au umefunga mjadala?
Bado naamini simba ni mbovu kwenye set pieces beki zinategeana kuruka mlandege na yosso boys sio kipimo sahihi cha kuisha tatizo.
 
Bado naamini simba ni mbovu kwenye set pieces beki zinategeana kuruka mlandege na yosso boys sio kipimo sahihi cha kuisha tatizo.
Namungo hujaiweka...au nayo si team ya kujilinganisha nao ...maana kuna team kubwa ili draw nao tena kwa chupli chupli ya refa
 
Ni siku nyingine tena na tatizo lile linalo jirudia la set pieces.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…