Salamu zangu!
Babu! Belgium naskia kuna mgao wa umeme! Huku hali ni shwari! Kuna mvua za elnino! Maji kibao mtera,kihansi,nyumba ya mungu! Umeme wa kutosha kabisa! Ila nadhani mafisadi ndo wanaupata, mana maeneo ya kama kule ninakoishi ni so!! Kiza kinene! Sema cha kushangaza ni kwamba bar bado zipo wazi! Kuhusu huo mgao wenu, kwa nini msiconvert hiyo snow kua maji kwa ajili ya kusukuma mitambo? Au kama ni nuclear umeme, nadhani mje kujenga mitambo huku kigoma karibu na colony la zamani kisha tunaupitisha bahari....au? Na sisi huku tupigane coz si hela za kigoma zitakuja kwa mafisadi dar!! Na kama jamaa wanaogopa terrorism kutoka kwa ndugu zetu wa pemba (wanyonge hawa) pale SUA kuna panya wa kudetect mabomu!! Kwa hiyo hiyo plant italindwa na panya!!! Ha! Jamani!!
Naskia pia mmeishiwa na nyama! Huku ipo nyingi sana! Yani ya kutosha! Ya kumwaga. Cha kushangaza ni kwamba, eti mifugo inakufa kwa njaa! Na pia kuna watu milioni moja wapo na janga la njaa! Inashangaza! Najiuliza, kwanini hii mifugo agalabu hafifu, kwa nini wasipewa wajanga hawa? Mana kwa sasa tunapoteza mifugu na watu!! Na mingine inapelekwa comoro! All the way from dodoma,shinyanga to comoro! Najiuliza tu jamani!! Sina uhakika kuhusu mchele umebaki kiasi gani!! Sijui. Ila najua tu kwamba pale ifakara pekee kuna ardhi na kila hali bora ya kutengeneza mchele kwa ajili ya Tanzania nzima na kuuza!! Nakupa mfano.....Kuna sehemu moja kame kuliko zote katika mkoa wa kilimanjaro. Ajabu ni kwamba....ndo wanatoa mchele wa kutosha kilimanjaro yote kwa kutumia maji ya mfereji! Kama kuna mtu anabisha aende Moshi, chekereni, kama kilometre 30 toka moshi mjini. Ofcoz pale kuna kitu kinaitwa Kilimanjaro Agricultural Training Centre!! Alas! ipo chini ya wajapan! wakishirikiana na maprofesa wa SUA. Maprofesa wetu ofcoz either wamechoka wakaingia katika politics wenyewe au hawasikilizwi kabisa inturn wanalisha familia zao tu!
Ulivokuja mara ya mwsho ulisema na huko kuna foleni ya kutosha!! Huku hakuna hata kidogo!! Yani kuna barabara nyingi kweli! Hasa maeneo ya oysterbay! Da! Kule bana....wameanza kurudishia lami ilioarabika ilowekwa na wakoloni zamani!! Sijui wamerudi? Sinza ninapoishi pia naisi itafika! Uchaguzi wa serikali za mitaa umefika! Ila naona mwaka huu wamechonga tu! kwa hiyo kuna vumbi kweli! Nimeskia kwamba wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2050 wataweka lami! Ninachotaka kusema ni kwamba barabara zetu ni kubwa sana! na zina nafasi za kutosha kabisa iloachwa kwa ajili ya kuongezewa indapo foleni itakua mbaya kama huko hata yakapita magari kumi kila upande! Sisi hatuna haja ya kujenga flyovers kama Ghana na Kenya ambao wameanza. Tuna ardhi ya kutosha sana! Mfano ni ule wa barabara tatu pale! Nafasi kubwa pande zote! Na sasa wanaongeza! Ila naona kuna baadhi ya majengo hawavunji! Kama lile la green acres business centre ambalo awali ilikua ni shule! BUT there demolishing the next building adjacent to it! Naiskia eti hiyo barabara inaenda alikotoka kiongozi wetu! Mana yule aliepita alitengeneza daraja na barabara ya kwenda kwake! Tungoje akitokea Kule kwenu ulikokimbia yeye atatengeneza itayolekea Rwanda in spirit of East africanism!
Ungependa kujua kuhusu hospitali zetu bora? Nitaliacha hilo na kuzungumizia habari za shule zetu na lugha ngeni ya kiingereza, Yani luga ya colonial masters wetu japo eti inasemekana wao walikua wakitutakecare! Kama umekua ukifatilia katika mitandao ambayo ni mingi kabisa na ya kutosha na hasa kama internet yako inatumia zile fibre optic cable za kupita baharini za spidi kali! Itakua ulimsikia kanumba akiwa katika lile jumba na kaka mkubwa!!! Inasemakana alisema nanukuu "...I am closing..." akimanisha he is "fasting" katika kile kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani! Sasa bwana, watanzania wacha wapate na hasira!!! wakamcheka! wakamzomea! Najiuliza.....watanzania hawa wamesoma shule zipi ambazo kingereza kilifundishwa vizuri hivo? Mana mimi nilikosoma kwa kweli hali haikua nzuri. Kwa maana ingine, kumcheka kanumba, ni kujicheka sisi wenyewe na mfumo wetu wa elimu! Ila kubwa zaidi, ni kudharau luga yetu ile baba wa taifa alituunganisha tukapata uhuru?
Sijui kama ungependa sana kuskia jinsi tumesherekea siku ya kufa kwa baba wetu wa taifa! Tulikaa nyumbani ofcoz!! Sina uhakika kama angekuepo angekubali hiyo hali au angesema tufanye kazi za jamii kama vile kusafisha mitaa yetu ambayo ni misafi kweli! haswa alikoamia lubango! Babu yangu aliwai niambia wakati wa bwana mkoloni, walikua wanatenga siku maalumu za kufanya kazi kwa mitaa ikiwepo usafi,kutengeneza barabara na mifereji ya maji ili jamii ipate!!! Ukienda utaona hadi leo hizi barabara zipo na mifereji! Najiuliza, hiyo sio muimu zaidi kipindi hiki cha uhuru? Tufanye kwa mapenzi ya taifa? Lakini huku kwetu ni kusafi zaidi!!!
Niishie hapo? Mmechoka? Mna kazi nyingi maofisini? Babu, una kipindi? Na nani? Moja ya wanafunzi? Au umetoka umekuja mjini kushulikia mishe mishe zako? Au sasa hivi upo unapata lunch! kisha ukirudi ofisini ni saa kumi! na mda wa kukaa ofisini umeisha??
Basi nimemaliza. Someni. Fanyeni kazi! Nawapenda wooooote! Sana! Labda kesho ikifika (taifa la kesho) sisi tutabadili mambo na kufanya nchi kua mbaya kama anayoishi Babu ambayo wamefanya ukatili kwa kutokomeza mmbu!! Kwa hiyo malaria hakuna!!! Wala Malale!!
Asenti
Courtesy of A. Kileo