SFO: Hivi ndivyo Chenge alihusika kashfa ya rada!

Naunga mkono kuwavalisha tairi kwani kiukweli hatuna vyombo vya sheria tena nchi hii!!!
 
Pia baba yake DR Hosea ndie aliemsomoshe Nimrod Mkono kupitia nafasi aliyekuwa nayo katika kanisa la kisabato ,kwa hiyo hawa wanasheria wa enzi hizo wanakamtandao kao akina Mkono,Hosea,Masaba,Chenge na mpwa Felesi.
mambo mengi sana yamejificha............tusipoangalia vizuri hizi background za viongozi wetu ndio chanzo cha mitandao michafu kama ya akina jk,lowasa,rostam
 
Pia baba yake DR Hosea ndie aliemsomoshe Nimrod Mkono kupitia nafasi aliyekuwa nayo katika kanisa la kisabato ,kwa hiyo hawa wanasheria wa enzi hizo wanakamtandao kao akina Mkono,Hosea,Masaba,Chenge na mpwa Felesi.
mambo mengi sana yamejificha............tusipoangalia vizuri hizi background za viongozi wetu ndio chanzo cha mitandao michafu kama ya akina jk,lowasa,rostam
 
Jamani, sijui Hosea anasema nini kufuatana na taarifa yake ya leo ya kummsafisha Chenge.
 
Mwenyewe kasema jalada lake la SFO na TAKUKURU yote yameshafungwa sasa hivi anasubiri ama kuapishwa au kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa Spika wa bunge la JMT
 
Mwenyewe kasema jalada lake la SFO na TAKUKURU yote yameshafungwa sasa hivi anasubiri ama kuapishwa au kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa Spika wa bunge la JMT


Tunataka nao SFO waseme -- maana hawajasema bado. Hata Takukuru walikuwa hawajasema bado. Mimi naona kuna uharaka unafanyika havya, yaani achaguliwe Uspika kabla SFO hawaja-confirm wanachodai Chenge na Hosea. SFO wakija na taarifa tofauti wakati Chenge kishakuwa spika ndiyo basi tena.
 
TAKUKURU wamesema Mh Chenge hahusiki-official statement from PCCB, ipo blog ya Michuzi
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA


Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.


TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.


Imetolewa na

Doreen J.
Kapwani,

Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010

S. L.P. 4865,

Dar Es Salaam.
http://www.wavuti.com/4/post/2010/1...ha-chenge-na-rada-takukuru.html#ixzz14hRxmHnW
 
Inasikitisha kuwa wtakuwa waandamizi wa serikali ya Tanzania. Labda ingefaa ya Albashir
 
Sasa hata kama alihusika mtafanya nini nyie watadanganyika? Kwanza hizo hela mbona kidogo tu ukilinganisha za kagoda?

Watanzania wengi hawahoji hizi tuhuma kwa nguvu. Watu walitakiwa waandamane nchi zima kushinikiza serikali isema ukweli kuhusu hizi hela. Lakini cha kushangaza watu kibao walikuwa wanachomwa na jua pale uwanja wa taifa jumamosi huku wakishangalia. Hawajuulizi hela za Kagoda alichukuwa nani na yuko wapi?

Wadanganyika bwana, kazi kweli.
 

Haya takukuru, mnajaribu lkutuchanganya makusudi au? Je hizo fedha ambazo serikali ya Uingereza imesema italipa kwa TZ na serikali yetu ikasema izipokee yenyewe nim za nini? Kama ni rushwa kwenye Rada nani alihusika kama siyo Chenge, Vithlan.Rashid na wenzao? Ebu tuwakumbushe taarifa ya SFO ambayo nyinyi takukuru mlikataa/mliogopa kuifanyia kazi:
 
Hosea's statement is unfair nonsense I tell you...:nono: What next? Lowassa and Aziz?
 
CHENGE KUWA SPIKA....NOOOOOOO!!
HOSEA KUMSAFISHA CHENGE ILI AWE SPIKA NOOOOOOOO!!
Ujanja-ujanja huu wananchi tusiupokee, tusiuafiki na tusiuvumile kamwe!
Hapa dawa ni wananchi kuandamana na kuupinga mpango huu wa kuikabidhi nchi kwa utawala unaotetea na kulinda mafisadi...
Hii haikubaliki, njama hapa ni kumuwezesha Chenge apite katika Uspika ili kuziba aina zote za kujadili haki za wananchi kuhusu ufisadi, ufilisi wa rasilimali na kulinda maslahi ya wanaotuhumiwa na watakaotuhumiwa kwa ufisadi...tutumbuke Richmond!

MUNGU IOKOE NCHI YETU INAYOPELEKWA KATIKA MAANGAMIZI....!
Nani hajui kuwa Richmond na Hosea alikuwepo? Rada nayo ina mikono ya vigogo? Hii ni hatari na haikubaliki...

Afadhali wananchi tulipinge lili kwa nguvu zote...hakuna cha Chenge kuwa Spika, na suala la Hosea kumsafisha ni ukiukwaji wa maslahi ya Taifa.
 
inasikitisha sana

yani ccm katika wale wabunge zaidi ya mia ndio wameona chenge anafaa?
 
TAKUKURU ni Chombo ambacho kinalinda maslahi ya Mafisadi wa Nchi hii. Taarifa zote na Ushahidi uliopo unajitosheleza hasa kuhusu jinsi Chenge na Rashid walipotajirika ghafula. TAKUKURU na Hosea wanataka kutuambia hawalioni hilo au ndiyo kuchakachua taaluma ili kulinda maslahi binafsi. Hosea awajibike. Lakini kama mtakumbuka wakati wa suala la RICHMOND, Bunge liliazimia Hosea awajibike lakini Ikulu ilimkingia kifua na hakujiuzulu. Tunahitaji wanasheria wa nchi hii waingilie kati kwa kuanzia pale SFO walipoishia ili watu aina ya hakina Chenge na Vikaragosi wao watendewe haki.
 

Kwa mtazamo wangu naona kesi hii inamizegwe kwani kuna watu mashuhuri ambao kwa namna fulani wanafununu za wizi huu kama wenyewe hawahusiki.

Jakaya Kikwete kama waziri wa mambo ya nje na sasa Rais
Bwana Othman Rashid kam afisa wa ubalozi uingereza na sasa mkurugenzi mkuu wa usalama
hawa nni watu mhimu sana katika kusaidia kupata mwafaka wa kesi hii lakini kama kwa namna fulani
walihusika au kuzembea wakati huo mnategemea mwenendo wa kesi uweje.
kama kampuni imekubali kulipa mamilioni hayo ni dhahili lisemwalo lipo.
Mwisho Hosea wa Tasisi ya kuzuia rushwa mnamtuma akazuie rushwa ipi?, hivi watanzania ni lini tutapata ufahamu ( Je utamtuma nyani kufukuza nyani wenzie kwenye shamba la mahindi mategemeo yako yatakuwa yepi?).
Lipo tazizo ambalo watanzania wengi bado tumelifumbia macho nalo ni la Uongozi bora,kama vile mwalimu Nyerere alivyowahi twambia kuwa tunahitaji Watu,Ardhi,siasa safi na uongozi bora, Watu tunao tena wavumilivu, Ardhi yetu imejaa neema ambayo haielezeki kiasi kuwa tuna hata madini yasiyopatikana kwingineko, vivutio k.m Kilimanjaro,Ngorongoro, Maziwa yetu makuu ambayo mengine ndo yanayochangia uhai wa baadhi ya nchi zingine kama Victoria inavyo watunza huko juu kwa mto Nile na n.k.Lakini uongozi bora haupo, hapo awali angalao tulikuwa na siasa safi sasa nayo imeyoyoma imebakia siasa ya samaki mkubwa kumla mdogo. Ndg zangu ni wakati wa kuamka na kuanza kupambana na uongozi huu dhaifu usio bora ambao una hatari ya kutusababishia janga na maafa yasiyo na sababu. Je tutakimbilia wapi maana nchi yetu ndo ya makimbilio sasa sisi tutakimbilia wapi.
 
Hivi wanasheria wa bongo inakuwaje mnakubali taaluma yenu inapakwa matope na ninyi mko kimya pride yenu iko wapi, jitokezeni basi tuone makali yenu, kila kitu ni magumashi kuanzia mikataba ya madini mpaka mienendo ya kesi, si mnamkumuka mlivyomuachia Zombe wakati ushahidi wa mazingira haukuwa na utata wowote, sasa mnataka tuwasifu kwa jema gani mlilolifanyia taifa lenu. kweli mnashangaza sana acheni upuuzi fanyeni kazi bwana, kama fani imewashinda nendeni mashambani mkaendeleze kilimo kwanza kwa power tilers za JK, mnaudhi sana kwa kweli, sijui mkoje? ???? :A S-baby: watu wengine bwana
 
zile pesa ni za watoto yatima na mimi ni mwanahisa tu.
full stop.
wenye wivu wajinyonge.
 
Wazungu nao siku hizi ni wasanii!mbona wamechelewa sana kutoa matokeo ya uchunguzi wao na hasa ukizingatia kwa sasa teknohama ipo juu sana ,hapa duniani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…