SGR imetutoa ushamba Wabongo, kila mtu anajipiga picha Station

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Watanzania sisi washamba hilo nimeligundua nilivyopanda usafiri wa Treni ya SGR. Tulivyoruhusiwa kutoka ndani station kwenda kupanda mabehewa ya treni kila mtu alitoa simu akaanza kujipiga ma photo mpaka mimi ni mmojawapo niliyejipiga picha aisee ama kweli Serikali inatutoa ushamba kupitia miradi ya maendeleo hatukuzoea, haya mambo tulikuwa tunayaona kwenye runinga tu.

Wenzetu South Africa wanayo miaka mingi mpaka wameyachoka, sasa hivi kuna watu hapa bongo wanasifiri ili tu kutoa ushamba wa Treni bila kuwa na jambo la msingi.
 
Imekutoa ushamba wewe ambae ndio mara ya kwanza kupanda treni. Kupiga picha ni tabia tu ya mtu hasa vijana wa sasa hivi wala sio ushamba.
 
Wenzetu South Africa wanayo miaka mingi mpaka wameyachoka, sasa hivi kuna watu hapa bongo wanasifiri ili tu kutoa ushamba wa Treni bila kuwa na jambo la msingi.
Hakuna ubaya wowote wa watu kuweka kumbukumbu zao kwa mambo yanayotokea kwa mara ya kwanza. Wapo wengi tu tulipiga picha tukiwa ndani ya ndege, au tukiwa nje ya nchi, tena tunatafuta sehemu yenye maandishi yatakayothibitisha hilo. Lakini baada ya muda na safari kuwa nyingi, linakuwa jambo la kawaida na picha hazipigwi tena
 
Watanzania sisi washamba hilo nimeligundua nilivyopanda usafiri wa Treni ya SGR. Tulivyoruhusiwa kutoka ndani station kwenda kupanda mabehewa ya treni kila mtu alitoa simu akaanza kujipiga ma photo mpaka mimi ni mmojawapo niliyejipiga picha aisee ama kweli Serikali inatutoa ushamba kupitia miradi ya maendeleo hatukuzoea, haya mambo tulikuwa tunayaona kwenye runinga tu.

Wenzetu South Africa wanayo miaka mingi mpaka wameyachoka, sasa hivi kuna watu hapa bongo wanasifiri ili tu kutoa ushamba wa Treni bila kuwa na jambo la msingi.
Sasa hapo mbona wewe ndiyo mshamba 🙄🙄 kwani kupiga picha ni tatizo tena kupiga picha jambo jema na lakupendeza biashara ni matangazo picha zina sambaa na kuwavutia nchi jirani kutia maanani kujenga reli kuunganisha na yetu ....mimi nasema wapige tu picha day and night
 
Ni kweli hakuna ubaya lakini nilichokuwa namaanisha ni mradi mpya kwetu sisi wa Tanzania, wa Tanzania wanashuhudia vitu walivyokuwa wakiona kwa mataifa ya wenzetu kwahiyo mradi unatoa watu ushamba mpaka wengine wanatengeneza tu safari zisizokuwa na ulazima ili tu wapate experience ya kupanda treni
 
Sasa hapo mbona wewe ndiyo mshamba 🙄🙄 kwani kupiga picha ni tatizo tena kupiga picha jambo jema na lakupendeza biashara ni matangazo picha zina sambaa na kuwavutia nchi jirani kutia maanani kujenga reli kuunganisha na yetu ....mimi nasema wapige tu picha day and night
Brother am just saying kwamba ni mradi mpya kwetu sisi wa Tanzania hatukuzoea kuwa na vitu vya kisasa. Try to understand me
 
Watanzania sisi washamba hilo nimeligundua nilivyopanda usafiri wa Treni ya SGR. Tulivyoruhusiwa kutoka ndani station kwenda kupanda mabehewa ya treni kila mtu alitoa simu akaanza kujipiga ma photo mpaka mimi ni mmojawapo niliyejipiga picha aisee ama kweli Serikali inatutoa ushamba kupitia miradi ya maendeleo hatukuzoea, haya mambo tulikuwa tunayaona kwenye runinga tu.

Wenzetu South Africa wanayo miaka mingi mpaka wameyachoka, sasa hivi kuna watu hapa bongo wanasifiri ili tu kutoa ushamba wa Treni bila kuwa na jambo la msingi.
Maisha hayataki ujuaji sana. Kupiga picha na treni kosa liko wapi? Watu wakivaa nguo au wakila msosi mzuri wanapiga picha sembuse Treni ya umeme? Kitu chochote kipya kinahitaji kumbukumbu tuache watu wawe huru na wala si ushamba
 
Back
Top Bottom